Vijana wa kizazi cha sasa maarufu kama Gen Z wameshauriwa kujifunza na kuenzi maadili ya vizazi vilivyotangulia maarufu ‘Wahenga”, ikielezwa kuwa kuwa maadili ni msingi wa maendeleo ya jamii kiuchumi na kitamaduni.
Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Mabadiliko ya Hatua kwa Hatua ya Binadamu (Anthropolojia), Marian Gichan amesema kuwa vizazi vya zamani vilijengeka katika misingi ya nidhamu na heshima kupitia mafunzo, simulizi na miiko iliyotolewa na wazee wa jamii.
Kwa mujibu wake, tofauti za vizazi husababishwa na mabadiliko ya mifumo ya maisha na maendeleo ya teknolojia, hali inayosababisha mitazamo, tabia na mienendo kubadilika kadri muda unavyopita.
✍Ibrahimu Kilumbo
Mhariri | @claud_jm
#AzamTVUpdates
(Feed generated with FetchRSS)