
Mahakama ya Morocco imetoa uamuzi wake siku ya Alhamisi, Februari 19, huko Rabat, wakati wa kumalizika kwa kesi ya mashabiki 18 wa Senegal na Mfaransa mmoja waliokamatwa wakati wa vurgugu zilizotokea wakati wa mchuano wa fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Morocco na Senegal. Wote walihukumiwa kifungo cha kuanzia miezi mitatu hadi mwaka mmoja. Mawakili wa pande wa utetezi wamebainisha kwamba watakata rufaa.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Watu hao walishtakiwa kwa “uhuni,” shtaka linalojumuisha vitendo vya vurugu, haswa dhidi ya vikosi ya ualama, uharibifu wa vifaa vya michezo, uwanja kuvamiwa, na kurusha vilipuzi.
Mapema alasiri, washtakiwa 19 walifika mahakamani wakiwa wawili wawili, wakiwa wamefungwa pingu. Chumba kidogo cha mahakama kilikuwa kimejaa watu. Mashabiki wa Senegal walisubiri uamuzi kwa saa kadhaa, anaripoti mwandishi wetu huko Rabat, mji mkuu wa Morocco, Matthias Raynal.
Tisa kati yao walihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela na kutozwa faini ya dirham 5,000 (takriban euro 460), wengine sita hadi miezi sita na faini ya dirham 2,000 (euro 180), na watatu wa mwisho walihukumiwa miezi mitatu na faini ya dirham 1,000 (euro 90).
“Haieleweki,” Patrick Kabou, wakili wao kutoka Senegal aliyesajiliwa katika chama cha mawakili wa Gers nchini Ufaransa, alisema kwa shirikala habari la AFP, akishutumu kwamba wateja wake wamefanyiwa tu unyonge.” Mfaransa mwenye asili ya Algeria, aliyeshtakiwa kwa kutupa chupa ya maji, alihukumiwa kifungo cha miezi mitatu jela na kutozwa faini ya dirham 1,000.
Wakili wake, Jaouad Benaissi, alisema alikuwa “mwenye huzuni na kukata tamaa” aliposikia uamuzi huo, ambao ulitolewa baada ya majadiliano yaliyodumu zaidi ya nusu saa. Baadhi ya mashabiki walionyesha kutoridhika kwao, mwandishi wa habari wa AFP amesema. Walisema watakata rufaa mapema Ijumaa.
Baada ya kusomwa kwa uamuzi huo, kelele zilisikika mahakamani. Baadhi ya washtakiwa walikataa kuondoka, na mmoja wao akazimia.
Mnamo Januari 18, wakati wa mchezo wa fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika huko Rabat, Senegal ilishinda 1-0 baada ya mechi iliyokumbwa na machafuko. Kufuatia adhabu iliyotolewa kwa Morocco katika kipindi cha pili cha mapumziko, mara tu baada ya bao kukataliwa kwa Senegal, mashabiki wa Senegal walijaribu kuvamia uwanja na kurusha vilipuzi uwanjani.
Mapema siku hiyo, upande wa mashtaka uliomba kifungo cha hadi miaka miwili jela kwa kila mmoja wao. “Walitaka kwa makusudi kuvuruga uendeshaji mzuri wa mechi” na “walifanya vitendo vya vurugu vilivyorushwa moja kwa moja kwenye vituo vya televisheni,” alisema mwendesha mashtaka wa umma. Kulingana na wakili wao, Patrick Kabou, wateja wake walifanya mwezi mmoja tu kizuizini kabla ya kesi kusikilizwa.