Askofu wa Kanisa la Ufunuo Tanzania, Paul Bendera ametoa ufafanuzi kuhusu umuhimu wa fungu la kumi kwa waumini, akisisitiza kuwa sadaka hiyo ya kiimani haipaswi kuhusishwa na fedha za mikopo.
Amesema fungu la kumi ni agizo la kiroho linalotolewa kwa hiari na kwa mapato halali aliyobarikiwa muumini, na si kwa fedha zilizokopwa au zilizo na masharti ya kurejeshwa.
Askofu Bendera ameeleza kuwa kuchanganya fungu la kumi na mikopo kunaweza kuleta mzigo wa kifedha na changamoto kwa waumini, badala ya kuleta baraka na ustawi wa kiroho. Amehimiza waumini kutoa kwa moyo wa shukrani kutokana na kipato chao halisi, bila kujitia katika madeni kwa ajili ya kutimiza ibada hiyo.
Aidha, amewataka viongozi wa dini kuendelea kutoa elimu sahihi juu ya utoaji ili kuepusha tafsiri potofu zinazoweza kuwaumiza waumini kiuchumi huku wakitekeleza imani yao.
#kilichoborakabisa
(Feed generated with FetchRSS)