#HABARI: Baraza la Ushindani Tanzania (FCT) limehimizwa kuziwezesha mamlaka zake za udhibiti kwa kuzipatia rasilimali watu na fedha za kutosha ili kuongeza ufanisi katika kutoa elimu kwa umma.

Katibu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Wilaya ya Mtwara, Leonard Peter, amesisitiza kuwa uwezeshaji huo utasaidia wananchi kuzitambua na kuzitumia mamlaka kama EWURA, LATRA, na TCRA kupata haki zao, badala ya kubaki kusoma mabango bila kuelewa utendaji wa taasisi hizo kisheria.

Matumizi ya teknolojia ya TEHAMA yatapewa kipaumbele na Baraza hilo ili kurahisisha upatikanaji wa haki na kupunguza usumbufu kwa jamii.

Afisa TEHAMA wa Baraza hilo, Athumani Kanyegezi, amebainisha kuwa wamejiimarisha kutoa elimu kwa umma kuhusu mifumo ya kidijitali, hatua inayomwezesha mwananchi kufungua na kufuatilia kesi zake kwa njia ya mtandao kutoka popote alipo bila kulazimika kufika ofisini.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *