#HABARI: Jeshi la Polisi kupitia Kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo Nchini (STPU), kwa kushirikiana na Shirika lisilokuwa la kiserikali la ASPA, limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa watatu waliokuwa wakitorosha mifugo aina ya Punda 21 kwenda Nchi jirani pasipo kuwa na kibali.
Kamanda wa Kikosi hicho, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Simon Pasua, ameyasema hayo Katika Kata ya Lengijave Mkoani Arusha, ambapo amesema kuwa upelelezi ukikamilika watuhumiwa hao watafikishwa Mahakamani kwa ajili ya hatua za Kisheria.
SACP Pasua amesema kuwa kutokana na Operesheni zinazofanywa na Kikosi hicho kote Nchini changamoto za usafirishaji wa mifugo bila kibali, zimepungua huku akiwataka Wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi kupitia Kikosi hicho katika kutokomeza Uhalifu Dhidi ya Mifugo.
Naye Afisa Mifugo Kata ya Lengijave Bwana Hedson Kindia, amesema kuwa wamekuwa wakazingatia uhalali wa umiliki na usafirishaji wa Mifugo katika Kata hiyo wakati wote PAMOJA na kulinda haki za Mifugo katika umiliki na Biashara.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania