#HABARI: Mwili wa Askofu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardanali Pengo unatarajiwa kuzikwa Jumamosi Februari 28, 2026 katika Kituo cha Hija Pugu jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Kanisa, shughuli za mazishi zitaanza Ijumaa Februari 27, 2026 ambapo mwili utawasili katika Kanisa Kuu la Mt. Yosefu kwa ajili kuuombea ikifuatiwa na mkesha wa sala na Maombolezo.
Jumamosi, mwili utaondolewa kanisani hapo na kuelekea Pugu kwa ajili ya watu kutoa heshima zao za mwisho kisha maziko kufanyika.