Jeshi la Polisi mkoani Arusha linaendelea na uchunguzi kuhusu kifo cha Abdilah Musa maarufu kwa jina la Banjo, kilichotokea Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, SACP Justine Masejo amesema walipokea taarifa ya kupotea kwa mtu huyo Februari 13, 2026, ikielezwa kuwa aliondoka nyumbani kwake tangu Februari 12, 2026.

Amesema wakati uchunguzi ukiendelea, Februari 19, 2026 walipokea taarifa za kifo chake mkoani Dodoma.

Kamanda Masejo ametoa wito kwa yeyote mwenye taarifa zinazoweza kusaidia uchunguzi huo kuziwasilisha kwa Jeshi la Polisi ili zichunguzwe na kufanyiwa kazi mara moja.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *