
Mahakama ya juu zaidi nchini Marekani imeamua kwamba rais wa Marekani alizidi mamlaka yake ya kikatiba kwa kuweka ushuru kwa karibu bidhaa zote zinazoingia nchini Marekani.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mahakama Kuu nchini Marekani imeamua baadhi ya ushuru uliowekwa na Donald Trump mwezi Aprili 2025 kuwa kinyume cha sheria.
Mahakama Kuu imeamua kwamba rais wa Marekani hakuwa na haki ya kutumia sheria ya 1977, IEEPA (Sheria ya Kimataifa ya Nguvu za Kiuchumi za Dharura), kutoza ushuru bila idhini ya Bunge.
Uamuzi huo umefikiwa na majaji sita walio wengi kwa watatu. Unahusu ushuru uliowasilishwa kama “wa pande zote” na Donald Trump, lakini sio ule unaotumika kwa sekta maalum, kama vile magari au chuma na aluminium.
Taarifa zaidi zinakujia…