Mwili wa Askofu Mkuu mstaafu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Cardinal unatarajiwa kuzikwa Jumamosi ya wiki ijayo Februari 28,2026.

Askofu huyo anatarajiwa kuzikwa eneo la kanisa lililopo Pugu Jijini Dar es katika kaburi alilojiandalia mwenyewe enzi za uhai wake.

Mara kadhaa Kardinali Pengo amekaririwa na vyombo vya habari akisema kuwa tayari ameshajiandalia kaburi eneo la Pungu na kuomba atakapo kufa azikwe katika kaburi hilo na si kwengine kwa sababu Dar es Salaam ndiyo sehemu aliyofanya kazi kwa muda mrefu zaidi licha ya kuzaliwa Sumbawanga na kufanya kazi mikoa mbalimbali ikiwamo ya kusini.

Kardinal Pengo ametwaliwa nyumbani kwa baba usiku wa kuamkia leo Ijumaa Februari 20,2026 akiwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Jijini Dar es Salaam.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *