Mzabuni Herbert Matiko Tugara kutoka Kampuni ya Herver General Services ameburuzwa mahakamani Kwa tuhuma za kutoa tuhuma za uongo na kugushi.

Tugara amefunguliwa kesi ya Jinai namba 3454/2026 katika Mahakama ya Wilaya ya Manyoni, mkoani Singida ambako anakabiliwa na shtaka la kutoa nyaraka za uongo kinyume na Kifungu cha 22 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Sura ya 329 (Marejeo ya mwaka 2022), pamoja na shtaka la kughushi kinyume na vifungu vya 333, 335(a) na 337 vya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 (Marejeo ya mwaka 2022).

Mshtakiwa anadaiwa kughushi risiti ya EFD yenye thamani ya Sh6,2 milionina kuiwasilisha kama nyaraka halali baada ya kupokea malipo ya kazi ya usambazaji wa vifaa vya umeme katika Hospitali ya Wilaya ya Manyoni iliyokuwa inakarabatiwa.

Mtuhumiwa huyo amesomewa mashtaka yake na Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Wilson Ntiro, mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Manyoni, Itika Koroso.

Hata hivyo, mtuhumiwa amekana mashtaka yanayomkabili na yupo nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti yaliyowekwa na mahakama. Kesi hiyo hiyo imepangwa Machi 2, 2026 kwa ajili ya kusoma hoja za awali na kuanza usikilizwaji.

#StarTvUpdate

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *