Jeshi la Nigeria limezindua rasmi operesheni kubwa ya kupambana na ugaidi siku ya Alhamisi katika Jimbo la Kwara katika eneo la katikati magharibi mwa nchi. Operesheni hii, iliyotangazwa mapema mwezi Februari, inakuja wakati wa kunaripotiwa ongezeko la ukosefu wa usalama unaosababishwa na magenge yenye silaha yanayojikita kwa utekaji nyara na wizi wa mifugo, pamoja na tishio linaloongezeka la wanajihadi, huku makundi yanayoendesha harakati zao kaskazini-magharibi mwa nchi yakienea kusini.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Lagos, Harmony Pondy Nyaga

Operesheni iliyopewa jina la Savannah Shield inalenga “kuvunja mitandao ya kigaidi, makundi ya utekaji nyara, na makundi yanayojihusisha na ukatili ambayo yanatishia Jimbo la Kwara na maeneo yake yanayozunguka,” makao makuu ya jeshi la Nigeria imesema katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Ili kuadhimisha tukio hilo, sherehe rasmi ya uzinduzi na ukaguzi wa wanajeshi ilifanyika katika kambi ya kijeshi ya Ilorin katika mji mkuu wa mkoa, ikihudhuriwa, miongoni mwa wengine, wakuu wa majeshi ya ulinzi na vikosi vya jeshi, pamoja na gavana wa jimbo la Kwara.

Gavana alielezea kutumwa kwa jeshi katika eneo hilo kama wa ” kimkakati, kwa wakati unaofaa, na wenye uhakika” dhidi ya kuibuka tena kwa tishio la kigaidi.

Zoezi la kutumwa kwa jeshi lilianza mapema mwzi Februari baada ya vifo vya watu 162 katika shambulio lililohusishwa na Boko Haram katika kijiji cha Woro katika Jimbo la Kwara.

Lakini tishio la usalama lenye pande nyingi linaathiri majimbo kadhaa nchini Nigeria. Siku ya Jumatano, kaskazini zaidi katika Jimbo la Kebbi, shambulio lililoratibiwa katika vijiji saba, lililohusishwa na kundi la wanajihadi huko Lakurawa, liliua watu 33.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *