Rais Samia Suluhu Hassan ametumia salamu za rambirambi kufuatia kifo Askofu Mkuu mstaafu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali, Pengo.

Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Bakari Machumu imesema kuwa Rais Samia amesimitishwa na kifo cha kiongozi huyo kilichotoke usiku wa kuamkia leo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).

“Katika kipindi chote cha utumishi wake, Kardinali Pengo alisimama imara katika kuhubiri amani, maadili na mshikamano wa kitaifa. Alikuwa sauti ya busara katika masuala ya kijamii na kimaadili, akihimiza amani, heshima na utu katika jamii yetu. Mchango wake katika malezi ya kiroho na maendeleo utaendelea kukumbukwa na kuenziwa siku zote.”.

“Ninatoa pole kwa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Wolfgang Pisa, Maaskofu, Mapadri, Watawa, familia, ndugu, jamaa, marafiki, waumini wa Kanisa Katoliki na Watanzania wote kwa msiba huu. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.”imesema sehemu ya taarifa hiyo.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *