Muswada huo uliyopitishwa na baraza la mawaziri jioni ya Jumatano, Februari 18, unalenga kuongeza adhabu kwa wale watakaopatikana na hatia ya “vitendo kinyume na maumbile” na kuzipanua kwa mashirika ambayo “yanakuza” mahusiano ya wapenzi wa jinsia moja. Sheria hii mpya bado inahitaji idhini ya bunge kabla ya kuanza kutumika.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Hii ilikuwa ahadi ya uchaguzi ya chama cha PASTEF, ambacho sasa kiko madarakani: nchini Senegal, muswada wa kukandamiza zaidi dhidi ya wapenzi wa jinsia moja ulipitishwa na baraza la mawaziri jioni ya Jumatano, Februari 18. Muswada huo ambao umependekezwa na serikali, unalenga hasa kuimarisha adhabu zilizoainishwa katika Kifungu cha 319 cha Kanuni ya Adhabu kwa wale watakaopatikana na hatia ya kile kinachoitwa “vitendo dhidi ya maumbile,” pamoja na kurekebisha ufafanuzi na kuzuia uendelezaji wa vitendo hivyo.

Ingawa sheria hii mpya inapendekeza kuongeza maradufu vifungo vya gereza—hadi miaka kumi—na kuongeza faini—ambazo zinaweza kufikia faranga milioni 10 za CFA, ikilinganishwa na faranga milioni 1.5 za sasa—ubunifu wake muhimu zaidi upo katika kupanua vikwazo hivi kwa yeyote atakayepatikana na hatia ya “kutetea” mahusiano ya wapenzi wa jinsi moja.

“Mashirika yote yanayojaribu kuhimiza, iwe kupitia filamu za propaganda, sinema, televisheni, au vifaa vya maandishi, falsafa ya LGBT—ambayo, nawakumbusha, ni ngeni kabisa kwa mila, mwenendo na utamaduni wa Senegal—yanahusika,” anaelezea Amadou Ba, Waziri wa Utamaduni wa Senegal, ambaye anabainisha kwamba sheria hiyo pia inajumuisha vikwazo dhidi ya “shutuma zozote za uwongo, ili mtu yeyote asilengwe kwa tabia ya kutiliwa shaka.” Mtu yeyote anayemtuhumu mtu binafsi kwa ushoga bila kutoa ushahidi atawajibika kwa kifungo cha miaka miwili hadi mitatu jela na faini ya faranga 200,000 hadi 500,000 za CFA.”

“Ubaguzi wa kisiasa”

Ingawa tangazo hili linakuja kama siku kumi baada ya kukamatwa kwa wanaume kadhaa wanaoshutumiwa kwa “vitendo visivyo vya asili” na maambukizi ya VVU kwa makusudi nchini, watu kadhaa wanapaza sauti zao kukemea “chuki” dhidi ya watu wa jamii ya LGBT nchini Senegal, anaripoti mwandishi wetu huko Dakar, Pauline Le Troquier.

Kabla ya kupitishwa kikamilifu, muswada mpya utalazimika kupigiwa kura na wabunge.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *