Serikali ya Senegal imeidhinisha muswada ambao kama utapasishwa na kuwa sheria, hatua hiyo itapelekea kupigwa marufuku vitendo vichafu vya mapenzi ya watu wa jinsia moja.

Muswada huo uliopitishwa na baraza la mawaziri unalenga kuongeza adhabu kwa wale watakaopatikana na hatia ya “vitendo vilivyo kinyume na maumbile” na kuzipanua kwa mashirika ambayo “yanashajiisha” mahusiano ya wapenzi wa jinsia moja. Sheria hii mpya bado inahitaji idhini ya bunge kabla ya kuanza kutumika.

Hii ilikuwa ahadi ya uchaguzi ya chama cha PASTEF, ambacho sasa kiko madarakani nchini Senegal. Muswada huo wa kukabiliana na vitendo vilivyo kinyume na maumbile vya wapenzi wa jinsia moja ulipitishwa na baraza la mawaziri jioni ya Jumatano, Februari 18.

Muswada huo ambao umependekezwa na serikali, unalenga hasa kuimarisha adhabu zilizoainishwa katika Kifungu cha 319 cha Kanuni ya Adhabu kwa wale watakaopatikana na hatia ya kile kinachoitwa “vitendo dhidi ya maumbile,” pamoja na kurekebisha ufafanuzi na kuzuia uendelezaji wa vitendo hivyo.

Ingawa sheria hii mpya inapendekeza kuongeza maradufu vifungo vya gereza—hadi miaka kumi—na kuongeza faini—ambazo zinaweza kufikia faranga milioni 10 za CFA, ikilinganishwa na faranga milioni 1.5 za sasa—ubunifu wake muhimu zaidi upo katika kupanua vikwazo hivi kwa yeyote atakayepatikana na hatia ya “kutetea” mahusiano ya wapenzi wa jinsi moja.

Mwaka 2024 nchi nyingine ya Kiafrika ya Ghana kupitia Bunge la nchi hiyo ilipasisha  muswada wa kupambana na ushoga na ubaradhuli, LGBTQ+ baada ya takriban miaka mitatu ya majadiliano.

Mataifa mengi ya Kiafrika yamekuwa yakipinga uchafu huu unaopigiwa debe na madola ya Magharibi yakisisitiza kwamba, hauendani na maadili, mila na tamaduni za Kiafarika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *