SIMBA inaendelea kujifua tayari kwa mechi mbili za Ligi Kuu Bara ikiwamo ya kesho Jumapili dhidi ya Tanzania Prisons, kisha Dodoma Jiji kabla ya kuifuata Yanga visiwani Zanzibar, lakini imebainika ni wachezaji wawili tu waliojihakikishia nafasi na kutumika chini ya makocha watano.

Wekundu hao walianza msimu ikiwa chini ya kocha Fadlu Davids na alipondoka timu ilishikiliwa kwa muda na Hemed Suleiman ‘Morocco’ na Seleman Matola, kabla ya kuletwa Dimitar Pantev na baadae Steve Barker aliyepo sasa, huku rekodi zikionyesha ni mabeki Shomary Kapombe na Rushine de Reuck pekee ndio waliotumika katika mechi nyingine chini ya makocha wote, tofauti na wenzao.

Kapombe diye mchezaji mwandamizi ndani ya kikosi hicho kwa sasa baada ya kuondoka kwa Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ aliyetua Yanga msimu huu ni nahodha wa timu hiyo, akisaidiwa na Rushine aliyejiunga Simba msimu huu akitokea Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Kwa mujibu wa mechi ambazo Simba imecheza msimu huu zikiwamo nane za Ligi Kuu Bara, moja ya Ngao ya Jamii na nyingine kama hiyo ya Kombe la Shirikisho (FA) na 10 za Ligi ya Mabingwa Afrika, Kapombe na Rushine ndio wanaoongoza kwa kutumika mechi nyingi wakiingia kikosi cha kwanza chini ya makocha wote waliinoa timu hiyo kuonyesha kukubalika kwao kwa kila kocha.

KAPO 01

Kapombe anayecheza kama beki wa kulia aliyerejea Msimbazi msimu wa 2017-2018 akitokea Azam FC sambamba na kipa Aishi Manula, kiungo Erasto Nyoni na mshambuliaji John Bocco ambao wote kwa sasa hawapo katika timu hiyo wakimuacha mkongwe huyo akiendelea kuibeba Simba.

Awali aliitumikia timu hiyo miaka ya 2010 kabla ya kwenda Ufaransa 2013 kucheza soka la kulipwa katik klabu ya Cannes na mwaka 2014 alirejea nchini na kutua Azam FC iliyokuwa imetoka kubeba taji la kwanza la Ligi Kuu Bara msimu wa 2013-2014.

Rushine naye tangu atue Msimbazi makocha wote walioinoa timu wamekuwa wakimpa nafasi kama ilivyo kwa sasa kwa Steve Barker anayemtumia zaidi na Wilson Nangu kabla yaa kuumia na kufaniwa upasuaji wa goti au na Ismael Toure aliyechukua nafasi ya Chamou Karaboue aliyekuwa akitumika na Msauzi. Lakini Rushine pia alikuwa akicheza na Abdulrazaq Hamza aliyeumia pia.

KAPO 02

Kwa upande wa Yusuf Kagoma ingawa bado ana nafasi kubwa kikosi cha kwanza, lakini ujio wa  Alasane Kante aliyejiunga na hiyo Julai 23,2025 akitokea klabu ya CA Bizertin, imekuwa kama chalenji kwake kuna wakati haanzi.

KINACHOWABEBA CHATAKWA

Aliyekuwa kocha wa Simba, Fadlu Davids ambaye kwa sasa anaifundisha Raja CA ya Morocco alisema: “Kapombe na Rushine ni miongoni mwa wachezaji wenye uwezo wa juu kwa wale ambao nimewafundisha Simba, wana nidhamu kubwa ya kazi yao.”

Staa wa zamani Yanga na Taifa Stars, Mohamed Hussein ‘Mmachinga’ alisema:”Kati ya sajili walizofanya Simba hivi karibuni ukiachana na waliyoingia dirisha dogo, Rushine ni beki mzuri na anawasaidia Simba pia sitaacha kumpa heshima yake Kapombe kwa kumenteini kiwango chake, kucheza muda mrefu Simba na Yanga siyo jambo la mchezo ni kwa mchezaji anayejielewa.”

KAPO 03

Staa mwingine wa zamani wa Yanga na Stars, Ally Mayay na mchambuzi wa soka nchini alisema:”Naheshimu ninapoona wachezaji wazawa wanalinda viwango vyao, nimekuwa nikisema mara nyingi kwamba Kapombe na Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ wanastahili heshima yao.”

DATA ZAO SHOMARI KAPOMBE

KMC (dk 90)

Petro Atletico (dk 40)

Esperance (dk 90) (bao 1)

Esperance (dk 90)

Mtibwa (dk 90)

Azam (dk 90)

Mbeya City (dk 60)

Stade Malien (dk 90)

Petro Atletico (dk 90)

JKT Tanzania (dk 90)

Yanga (dk 90)

Gaborone (dk 90)

Fountain Gate (dk 72)

Namungo (dk 90)

Gaborone (dk 90)

Nsingizini (dk 90)

KAPO 04

RUSHINE DE REUCK

Stade Malien (dk 90)

KMC (dk 90)

Petro Atletico (dk 90)

Esperance (dk 90)

Esperance (dk 90)

Mtibwa (dk 90)

Stade Malien (dk 45)

Petro Atletico (dk 90)

JKT Tanzania (dk 90)

Yanga (dk 90)

Gaborone (dk 90)

Fountain Gate (dk 72) bao 1

Namungo (dk 90) bao 1

Gaborone (dk 90)

Nsingizini (dk 90)

YUSUF KAGOMA

Stade Malien (dk 90)

KMC (dk 90)

Petro Atletico (dk 90)

Esperance (dk 58) (bao 1)

Esperance (dk 90)

Azam (dk 90)

Mbeya City (dk 90)

JKT Tanzania (dk 90)

Yanga (dk 90)

Fountain Gate (dk 64)

Namungo (dk 90)

Gaborone (dk 90)

Nsingizini (dk 25)

Nsingizini (dk 90)

ALASANE KANTE

Stade Malien (dk 70)

Petro Atletico (dk 51)

Esperance (dk 74)

Azam (dk 84)

Mbeya City (dk 79)

Stade Malien (dk 45)

Petro Atletico (dk 84)

JKT Tanzania (dk 64)

Yanga (dk 54)

Fountain (dk 45)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *