Zaidi ya raia 640 wa Uholanzi wamehudumu katika jeshi la Israel wakati wa vita vya mauaji ya halaiki vya utawala huo wa Kizayuni dhidi ya Gaza na kwneye mashambulizi dhidi ya Ukingo wa Magharibi, takwimu mpya zinaonyesha, huku wataalamu wa sheria wakionya kwamba, wale waliohusika wanaweza kushtakiwa chini ya sheria za kimataifa na za nchi hiyo za uhalifu wa kivita.

Takwimu mpya zilizotolewa na jeshi la Israel zinaonyesha kwamba, angalau wanajeshi 645 waliokuwa wakihudumu mwezi Machi 2025 walikuwa na uraia wa Israel na Uholanzi, huku zaidi ya 80 wakiwa na uraia wa tatu, lakini haijulikani wazi kama wanajeshi wa akiba wasiohudumu walijumuishwa.

Takwimu tofauti kutoka kwa mashirika ya kutoa misaada yenye makao yake Marekani zinaonyesha kwamba, angalau raia 21 wa Uholanzi walisafiri mahususi kutoka Uholanzi kuhudumu kama “askari pekee” ikimaanisha walijiunga kwa uhuru bila wazazi huko Israel.

Maeneo ya huduma ya wanajeshi hawa – iwe Gaza, ardhi zilizokaliwa kwa mabavu 1948, au Ukingo wa Magharibi uliokaliwa kwa mabavu – bado hayajabainishwa.

Siku chache zilizopita, ripoti iliyochapishwa na ‘Declassified UK’ ilifichua kwamba, zaidi ya raia 2,000 wa Uingereza walipigana pamoja na vikosi vya utawala wa Israel wakati wa vita hivyo vya mauaji ya kimbari huko Gaza.

Mnamo 2025, zaidi ya wanajeshi 3,700 kutoka nchi 70 waliripotiwa kuhudumu katika jeshi la Israel, jambo linaloonyesha ushiriki wa kimataifa katika mauaji ya kimbari ya Gaza.

Mashirika mbali mbali ya kutetea haki yamekuwa yakishinikiza kufuatiliwa watu waliohusika katika vita vya mauaji ya kimbari vya utawala wa Israel dhidi ya Gaza, ambavyo vilianza Oktoba 2023, na ambavyo mpaka sasa vimesababisha zaidi ya Wapalestina 75,000 kuuawa shahidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *