Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umemtambulisha rasmi mkandarasi atakayetekeleza mradi wa kusambaza umeme katika vitongoji 474 vya Mkoa wa Kagera, ambapo utekelezaji wake unatarajiwa kuanza Februari 2026 hadi Februari 2029.
Akizungumza wakati wa kutoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo, Meneja Miradi Kanda ya Ziwa kwa niaba ya Meneja Mkuu wa REA, Ernest Makale, amesema kuwa Mkoa wa Kagera una jumla ya vijiji 662 na vyote tayari vimeunganishiwa huduma ya umeme.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Yahaya Ramadhani Kido, amewataka wakandarasi watakaohusika na utekelezaji wa mradi huo kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na kwa kasi ili kukidhi mahitaji makubwa ya umeme kwa wananchi, hususan wanaoishi vitongojini. Amesisitiza kuwa upatikanaji wa umeme ni kichocheo muhimu cha maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika mkoa huo.
(Feed generated with FetchRSS)