Watuhumiwa saba wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro wakikabiliwa na mashtaka ya kujihusisha na dawa za kulevya aina ya mirungi.

Kwa mujibu wa taarifa za mahakama, kesi saba zimefunguliwa, kila moja ikiwa na mtuhumiwa mmoja.

Watuhumiwa wote walisomewa mashtaka yao na walikana tuhuma zinazowakabili, na mashauri yao kupangiwa tarehe nyingine.

#AzamTVupdates
✍Estabela malisa
Mhariri | John Mbalamwezi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *