SONGWE: Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Farida Mgomi, ametoa rai kwa wananchi kujenga utamaduni wa kujitolea damu kwa hiari ili kuokoa maisha ya wajawazito na watoto wachanga wanaohitaji huduma za dharura.

DC Mgomi ametoa kauli hiyo wakati akifungua kikao kazi cha siku mbili cha mapitio ya vifo vitokanavyo na uzazi na vifo vya watoto wachanga kwa Mkoa wa Songwe kilichowakutanisha wataalamu wa afya kutoka wilaya zote za mkoa huo.

Amesema upatikanaji wa damu salama na ya kutosha ni moja ya nyenzo muhimu katika kupunguza vifo vinavyoweza kuzuilika, na akasisitiza kuwa utoaji damu ni tendo la upendo na uzalendo linalopaswa kupewa kipaumbele kama ilivyo sadaka katika nyumba za ibada.

Aidha, amewataka wataalamu wa afya kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa uchangiaji damu wa hiari ili kuhakikisha vituo vya afya vinakuwa na akiba ya kutosha muda wote kwa ajili ya dharura.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *