
Ghana ambayo imekitaja miaka minane ya mazungumzo yasiyo na matunda, imetangaza siku ya Ijumaa, Februari 20, kusitisha mazungumzo na Lomé yanayolenga kusuluhisha mzozo kati ya nchi hizo mbili kuhusu mpaka wao wa baharini. Accra imeamua kupeleka kesi hiyo katika Mahakam ya Kimataifa ya Sheria ya Masuala ya Bahari.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Accra, Victor Cariou
Ofii ya rais wa Ghana ilitangaza katika taarifa iliyotolewa siku ya Ijumaa, Februari 20, kwamba katika mzozo na Togo kuhusu mpaka wao wa baharini, Accra imeamua kusitisha mazungumzo na Lomé na kutumia usuluhishi wa kimataifa, “kulingana na Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Sheria ya mauala ya Bahari.” Mamlaka ya Ghana inakusudia “kuepuka kuongezeka kwa matukio yanayosababisha mvutano uliochochewa kati ya baadhi ya taasisi fulani” za nchi hizo mbili.
Uamuzi wa Ghana unategemea ukweli kwamba hakuna makubaliano kuhusu mzozo huu zamani wa nusu karne ambayo yangeweza kufikiwa baada ya miaka minane ya mazungumzo kati ya majirani hao wawili. Majadiliano yalianza mwaka wa 2018 na kuundwa kwa kamati ya awali. Kuanzishwa kwake kulitokana na changamoto ya Togo kuhusu uhalali wa mpaka uliopo—urithi wa kipindi cha ukoloni.
Mgogoro ulianza kati ya Ghana na Cote d’Ivoire
Mikutano mingi ilifuata, ambayo yote iliishia kushindwa. Mnamo mwaka 2021, Lomé ilikataa pendekezo la Ghana la kuanzisha mpaka wa muda, kwani Ghana ilikuwa tayari inatumia sehemu ya eneo lenye mgogoro. Ingawa mkutano kati ya wakuu wa nchi wa Togo na Ghana ulifanyika mwaka uliofuata, hakuna maendeleo makubwa yaliyoonekana kufanywa tangu wakati huo.
Kabla ya Togo, mgogoro kama huo ulikuwa kati ya Ghana na Côte d’Ivoire hadi mwaka 2017. Mahakama ya Kimataifa ya Sheria ya Masuala ya Bahari hatimaye ilisuluhisha mgogoro huo, ikitoa uamuzi kwa niaba ya Accra.