
Kwa siku nane za mashindano ya mbio za baisikeli, toleo la kumi na nane la Tour du Rwanda litafanyika kuanzia Februari 22 hadi Machi 1. Mbio hizo zitaanzia Rukomo na kumalizika katika mji mkuu, Kigali, ambao uliandaa Mashindano ya Dunia mwezi Septemba mwaka uliyopita.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Miongoni mwa uvumbuzi mashuhuri wa toleo hili la mwaka 2026, wilaya ya Rubavu itakuwa mwenyeji wa mashindano haya kwa siku tatu mfululizo, ikiwa ni pamoja na jukwaa kwenye mzunguko wa jiji, lkwa mara ya kwanza kwa mashindano ya mbio hizo.
Waendeshaji watawasili Rubavu wakati wa hatua ya 4. Siku inayofuata, watashindana katika mzunguko wa jiji wa kilomita 82 na mita 888 za kuongezeka kwa mwinuko. Washiriki kisha wataondoka Rubavu kwenda Musanze kwa hatua inayofuata.
Kwa hivyo, mashindao ya mbio za baiikeli ya Tour du Rwanda ya 2026 yatakuwa na hatua mbili za mzunguko: moja huko Rubavu na nyingine wakati wa hatua ya mwisho huko Kigali. Hatua ya mwisho itakumbusha Mashindano ya Dunia ya 2025, ambapo itaanza na kumalizika katika Kituo cha Mikutano cha Kigali. Kwa ratiba: kilomita 99 na mita 2,092 za kupanda mwinuko.
Timu tatu za taifa kutoka Afrika mwanzoni
Timu mbili za maendeleo za WorldTour, Timu ya Movistar (Uhispania) na NSN (Uswisi), ambayo zamani ilikuwa Israel Premier Tech, zitajiunga na washiriki wa Tour du Rwanda kwa mara ya kwanza. Swift Pro Cycling pia itashiiki mashindano hayo, na kuwa timu ya kwanza ya Brazil kushiriki katika mbio hizo. Mtaalamu wa zamani wa baiskeli za milimani Henrique Silva Avancini ni miongoni mwao.
Timu tatu za taifa zitawakilisha bara la Afrika: Rwanda, Eritrea, Ethiopia, na timu ya wataalamu ya Afrika Kusini. Timu mchanganyiko ya Afrika pia itakuwepo mwanzoni, akiwemo Issiaka Cissé kutoka Côte d’Ivoire. Patrick Yukusenge atashiriki katika kwa mara ya kumi na nne kwa timu ya Rwanda.
Kwa upande wa Ufaransa, kutakuwa na wawakilishi wawili tu kutoka timu ya BIKE AID: Baptiste Huyet na Victor Vidal.
Njia:
Hatua ya kwanza (22/02): Rukomo – Rwamagana (174km)
Hatua ya pili (23/02): Nyamata – Huye (kilomita 135)
Hatua ya tatu (24/02): Huye – Rusizi (kilomita 145)
Hatua ya nne (25/02): Karongi – Rubavu (kilomita 127)
Hatua ya tano (26/02): Rubavu – Rubavu (km 82)
Hatua ya sita (27/02): Rubavu – Musanze (km 84)
Hatua ya saba (28/02): Musanze – Kigali (km 147)
Hatua ya nane (01/03): Kigali – Kigali (km 99)