Maoni ya umma nchini Marekani katika mwaka huu wa 2026, yanapinga vikali chokochoko yoyote mpya ya kijeshi dhidi ya Iran. Fikra za walio wengi nchini Marekani zina mtazamo hasi kuhusiana na sera za kupenda vita za Rais mtata Donald Trump.

Kulingana na Pars Today, huku Rais wa Marekani mwenye utata Donald Trump na baadhi ya watu wenye msimamo mikali huko Washington wakipiga ngoma ya vita dhidi ya Iran, matokeo ya uchunguzi mpya wa maoni hivi karibuni nchini Marekani yanaonyesha picha tofauti kabisa ya maoni ya umma nchini humo. Tofauti na Machi 2003, wakati uvamizi wa Marekani dhidi ya Iraq ulipoungwa mkono na 72% ya Wamarekani (kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni wa Gallup), sasa maoni ya umma ya Wamarekani kwa kiasi kikubwa yanasema “hapana” kuanzisha vita vingine huko Asia Magharibi.

Kulingana na uchunguzi wa maoni wa pamoja wa Chuo Kikuu cha Maryland-SSRS uliofanyika mapema Februari 2026, ni asilimia 21 pekee ya Wamarekani ndio wanaounga mkono shambulio la kijeshi dhidi ya Iran. Hii ni katika hali ambayo, asilimia 49 wanapinga waziwazi hatua yoyote ya kijeshi, na asilimia 30 hawajaamua. Takwimu hizi zinalinganishwa vyema na chunguzi za maoni zilizofanywa baada ya mashambulizi ya Juni 2025 (ambapo asilimia 85 walipinga vita na Iran), ikionyesha mwenendo unaoendelea wa upinzani mkubwa dhidi ya vita nchini Marekani.

Nukta ya kuzingatiwa ni kwamba, hakuna makubaliano ya vita hata ndani ya kambi ya chama cha Republican. Ingawa chama hicho kinaonyesha mwelekeo mkubwa zaidi kuelekea chaguo la kijeshi kwa asilimia 40, lakini asilimia 25 ya wapiga kura wa Republican wanapinga vita na asilimia 35 hawana msimamo wawazi kuhusiana na hilo.

Matokeo haya yametambuliwa hapo awali katika chunguzi mbalimbali za maoni nchini Marekani. Ukweli wa mambo ni kuwa, chunguzi nyingi za maoni katika miezi ya hivi karibuni zinaonyesha kwamba, jaribio la “uingiliaji wa kijeshi wa Marekani” limeshindwa vikali:

Katika uchunguzi wa maoni wa Economist/YouGov uliofanyika mwishoni mwa Januari 2026, asilimia 48 ya Wamarekani walipinga hatua za kijeshi dhidi ya Iran, ikilinganishwa na asilimia 28 waliounga mkono. Walipoulizwa kuhusu “kuwaunga mkono waandamanaji”, upinzani uliongezeka hadi asilimia 52.

Pia, kulingana na uchunguzi wa maoni wa Chuo Kikuu cha Quinnipiac uliofanywa mapema Januari 2026, wiki moja baada ya Trump kutishia kuwa “yuko tayari na amejizatiti kwa silaha,” asilimia 70 ya waliohojiwa walisema, Marekani haipaswi kuingilia masuala ya ndani ya Iran, na asilimia 18 pekee ndiyo iliyounga mkono kuingilia masuala ya ndani ya Iran.

Wachambuzi wanasema kuwa, kumbukumbu chungu ya Vita vya Iraq imeleta kivuli kizito kwenye mawazo ya sasa ya Wamarekani. Katika maadhimisho ya miaka 20 ya uvamizi wa Iraq, asilimia 61 ya Wamarekani waliona uvamizi huo kama kosa kubwa. Baadhi ya wachambuzi wanaamini kwamba, sababu ya Trump hadi sasa kujizuia kushambulia Iran ni kwamba, tofauti na Rais wa wakati huo George W. Bush mwaka wa 2003, hakuna kampeni kubwa ya matangazo iliyofanikiwa kujenga uungaji mkono wa umma na Chama cha Republican pia kimegawanyika. Zaidi ya hayo, matokeo ya chunguzi hizi za maoni yanaweza kuwa na nafasi katika uamuzi wake katika suala hili.

Inaonekana kwamba, upinzani mkubwa wa watu wa Marekani dhidi ya uchochezi wa vita wa Trump unatokana na sababu thabiti zinazotokana na uzoefu mchungu wa kihistoria.

Sababu moja ya hili ni uchovu mkubwa wa “vita visivyo na mwisho” vya Marekani katika karne ya 21. Kimsingi ni kuwa, sababu muhimu zaidi ya upinzani wa umma ni kumbukumbu chungu ya miongo miwili ya vita nchini Afghanistan na Iraq. Wamarekani wamegundua kuwa vita hivi si tu kwamba, havikuwahakikishia usalama wao, bali pia viligharimu matrilioni ya dola na kuwaacha maelfu wakiwa wamekufa na kujeruhiwa. Tofauti na mwaka wa 2003, wakati asilimia 72 ya umma iliunga mkono uvamizi wa Iraq, leo ni asilimia 21 tu ndio wanaounga mkono kurudia kosa kama hilo. Watu waliwapa kura wanasiasa walioahidi kukomesha vita hivi lakini sasa wanasiasa hao wanafikiria kuanzisha vita vipya.

Sababu nyingine ni hofu ya majibu ya Iran na kuwaka moto katika kanda nzima. Kinyume na dhana iliyoenea, umma wa Marekani unaipa uzito maalumu nguvu ya kijeshi ya Iran na uwezo wake wa kujibu kwa uzito mkubwa shambulio la kijeshi dhidi yake. Matokeo ya uchunguzi wa maoni yanaonyesha kwamba, karibu asilimia 80 ya umma una wasiwasi kuhusu vita vikali na majibu ya Iran. Uwepo wa vituo kadhaa vya Marekani jirani na Iran na uwezo mkubwa wa makombora wa nchi hiyo umeongeza wasiwasi kwamba, shambulio lolote litagharimu maisha ya wanajeshi wa Marekani na usalama wa washirika wa kikanda.

Sababu ya tatu ni kutoaminiwa serikali ya Marekani na ukosefu wa uwazi. Utawala wa Trump umeshindwa kutoa uhalali wa kushawishi shambulio hili. Kwa upande mmoja, unadai “umeharibu kabisa” mpango wa nyuklia wa Iran katika mashambulizi ya mwaka jana, na kwa upande mwingine, unatumia mpango huo huo kama kisingizio cha vita mpya. Utata huu na kutokuweko mjadala wowote mzito na kura katika Bunge la Marekani umeimarisha dhana hii kwamba, Ikulu ya Marekani inatafuta vita visivyo vya lazima tena bila idhini ya kisheria.

Sababu nyingine ni ulazima wa vipaumbele vya ndani kuliko uvamizi wa kigeni. Wapiga kura wa Marekani, hasa katika hali ya sasa ya kiuchumi, wanataka serikali yao iangazie matatizo ya ndani kama vile mfumuko wa bei na kuupanda gharama za maisha, na kuona mabilioni yoyote yanayotumika kwenye vita mpya kama kinyume na maslahi ya kitaifa. Hata miongoni mwa Warepublican wenyewe na kambi ya “Marekani Kwanza”, kuna imani kubwa kwamba vita na Iran si tu kwamba, havitatimiza tu kauli mbiu ya “Marekani Kwanza”, vitaitumbukiza nchi hiyo kwenye kinamasi kipya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *