
Waziri wa Ulinzi wa Pakistan amesisitiza kwamba, suala la kuutambua rasmi utawala wa Kizayuni wa Israel si jambo ambalo lipo katika ajenga za nchi hiyo.
Khawaja Asif Waziri wa Ulinzi wa Pakistan amesema hayo katika mahojiano na France 24 ambapo alibainisha kwamba, uwezekano wa kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Islamabad na utawala wa Kizayuni unaoua watoto.
Ameongeza kwa kusema: Ikiwa Wapalestina wataanzisha taifa huru, anaweza kufikiria hatua hii.
Alipoulizwa kama Pakistan “itaanzisha uhusiano wa kawaida na Wazayuni kama nchi zingine za Kiislamu, Waziri wa Ulinzi wa Pakistan alijibu: “Sioni hata kama chaguo hili limezingatiwa na Pakistan.”
“Kuutambua rasmi utawala wa Kizayuni wa Israel ni jambo ambalo haliko kabisa katika ajenda za Islamabad, amesisitiza waziri huyo wa ulinzi wa Pakistan.
Ikumbukwe kuwa, Ijumaa ya tarehe 23 Oktoba, 2020 Rais wa wakati huo wa Marekani Donald Trump alitangaza kuwa Sudan na Israel zimefikia mapatano ya kuanzisha uhusiano wa kawaida ikiwa na maana ya Sudan kujiunga na nchi zingine za Kiarabu na Kiislamu za Misri, Jordan, Imarati na Bahrain kuutambua rasmi utawala huo haramu unaoikalia kwa mabavu Palestina na Quds tukufu.
Nchi kadhaa za Kiarabu zimeamua kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel ilhali kwa miaka na miaka sasa utawala huo wa Kizayuni umekuwa ukiendeleza jinai na ukandamizaji dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina na kuyakalia kwa mabavu maeneo mengi ya ardhi za nchi za Kiislamu na Kiarabu.