Darwin Nunez

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 2

Tottenham na Newcastle wana shauku ya kumrudisha kwenye ligi kuu mshambuliaji wa Al-Hilal wa Uruguay mwenye umri wa miaka 26, Darwin Nunez, ambaye zamani alikuwa Liverpool. (Teamtalk)

Tottenham na Aston Villa ni miongoni mwa vilabu vinavyomfuatilia kiungo wa Lyon wa Jamhuri ya Czech mwenye umri wa miaka 25, Pavel Sulc. (Mail)

Beki wa Uingereza Joe Gomez anaonekana kujiandaa kuondoka Liverpool msimu huu wa joto huku AC Milan na Bayern Munich wakipendezwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28. (Caught Offside)

Joe Gomez

Chanzo cha picha, Getty Images

Roma na Juventus wamejiunga na kinyang’anyiro cha kumsajili beki wa Argentina wa Bournemouth mwenye umri wa miaka 28, Marcos Senesi mwishoni mwa msimu. (Corriere Dello Sport)

Real Madrid wanaongoza kinyang’anyiro cha kumsajili beki wa Ujerumani wa Borussia Dortmund, Nico Schlotterbeck, lakini Barcelona pia wana hamu ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26. (AS)

Newcastle wana shauku ya kumsajili beki wa Uhispania mwenye umri wa miaka 23, Hugo Bueno kutoka Wolves msimu huu wa joto. (Football Insider)

Hugo Bueno

Chanzo cha picha, Getty Images

Liverpool inaandaa dau la pauni milioni 83 kwa winga wa Newcastle mwenye umri wa miaka 24 wa Uingereza Anthony Gordon ikiwa mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah, 33, ataondoka klabuni msimu huu wa joto. (Fichajes)

Everton wanatarajiwa kutoa dau la pauni milioni 30 kwa mshambuliaji wa Chelsea mwenye umri wa miaka 23 wa Uingereza Liam Delap msimu huu wa joto. (Teamtalk), nje

Crystal Palace wanajaribu kumshawishi Gareth Southgate kuchukua nafasi ya Oliver Glasner kwa msingi wa meneja wa muda hadi mwisho wa msimu. (Football Insider)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *