Utendaji duni wa Bandari ya Karema, unaochangiwa na kutokukamilika kwa miundombinu ya barabara, umetajwa kuwa sababu ya kusafirishwa kwa tani 15,000 pekee za mizigo tangu kuanza kwa utekelezaji wa shughuli zake mwaka 2022.

Changamoto kubwa imetajwa kuwa ni barabara kutoka Mpanda hadi Karema ambayo bado haijakamilika, hali inayokwamisha usafirishaji wa mizigo kwa ufanisi kutoka maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya Mkoa wa Katavi.

Kufuatia hali hiyo, Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile amesema Serikali imetenga zaidi ya shilingi bilioni 300 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya reli kutoka Kaliua hadi Mpanda, hatua inayolenga kuimarisha mtandao wa usafirishaji na kuongeza ufanisi wa bandari hiyo.

✍ Mwanaidi Waziri
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *