Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen, ameashiria kile kinachojulikana kama “Bodi ya Amani ya Trump” kwa ajili ya Gaza, na kusema: “Marekani ni mshirika wa adui Mzayuni katika jinai zake zote.”

Kwa muujibu wa Shirika la Habari la Mehr, likinukuu Al-Masirah, Sayyed Abdul Malik al-Houthi,Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema katika hotuba yake: “Maadui wanazidi kulenga maeneo matakatifu ya Kiislamu, hasa Msikiti wa Al-Aqswa, na hivi karibuni wameweka vikwazo vipya dhidi ya kuingia waumini katika msikiti huu mtakatifu.”

Kiongozi wa Ansarullah aliita kitendo hiki “hatua ya uadui na hatari sana” na akasisitiza kwamba kuweka kikomo na idadi maalum kwa waumini katika Msikiti wa Al-Aqswa ni ukiukaji wa wazi wa uhuru wa kuabudu na kitendo cha uchochezi dhidi ya umma wa Kiislamu.

Al-Houthi alisisitiza kwamba lengo kuu la Wayahudi ni kuharibu Msikiti wa Al-Aqsa na kuuharibu kama ishara takatifu ya Kiislamu na kuubadilisha na “hekalu lao linalodaiwa.”

Aliongeza: “Maadui wanajaribu kulifikisha taifa hili katika hatua ya kutojali ili jambo hatari zaidi litokee.”

Kiongozi wa Harakati ya Ansar Allah amebainisha kuwa, mauaji ya kila siku huko Gaza hayajakoma, na mabomu dhidi ya majengo, hali ya njaa, na kuzingirwa kwa ukanda huo kunaendelea.

Akiendelea na hotuba yake, Al-Houthi aliashiria kiburi cha wazi chaa Wayahudi-Wamarekani dhidi ya Palestina, na akazingatia tumaini pekee na njia ya wokovu kwa taifa hili kushikamana na Mungu, akisisitiza kwamba njia zingine ni za uharibifu na ni kupoteza muda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *