Kiongozi wa chama cha Union for Reason and Justice cha Ujerumani, Sarah Wagenknecht, anatoa wito kwa serikali ya nchi yake kuondoa vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Iran na kuzuia Marekani kutumia kambi za kijeshi nchini Ujerumani kuanzisha mashambulizi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.

 Sarah Wagenknecht ameandika kwenye akaunti yake ya mitandao ya kijamii: “Serikali ya Ujerumani sasa lazima itumie njia zote za kidiplomasia kuzuia vita na kufikia suluhisho kwa njia ya mazungumzo. Miongoni mwa hatua muhimu ni kuondoa vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Iran ili kuwezesha mazungumzo na kuzuia hali isizidi kuwa mbaya kwa watu wa Iran. Zaidi ya hayo, serikali lazima izuie Marekani kutumia kambi zake za kijeshi nchini Ujerumani ili kuunga mkono vita dhidi ya Iran.”

Wagenknecht amesisitiza haja ya kuzuia ongezeko lolote la mvutano kati ya Marekani na Iran kwa gharama yoyote ile.

Kiongozi wa chama cha Union for Reason and Justice cha Ujerumani amesema kwamba Marekani ina nia ya kubadilisha utawala nchini Iran, “kwa sababu uongozi wa sasa wa nchi hiyo ya Mashariki ya Kati unapinga ushawishi wa kisiasa na kiuchumi wa Marekani.”

Wagenknecht amehitimisha kwamba “demokrasia haiwezi kuanzishwa kupitia mashambulizi ya mabomu.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *