Mahakama ya Madagascar inaendelea na uchunguzi wake kuhusu Mamy Ravatomanga, mfanyabiashara mkubwa na mshirika wa karibu wa rais aliyetimuliwa madrakani Andry Rajoelina, ambaye kwa sasa yuko kizuizini kabla ya kesi nchini Mauritius kwa utakatishaji fedha na kula njama. Siku ya Jumamosi, kitengo cha kupambana na ufisadi huko Antananarivo kilitangaza kuwa kimetoa waranti mpya wa kumatwa dhidi yake.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Antananarivo, Guilhem Fabry

Kesi hii, inayowahusisha majaji wanne wanaochunguza mashitaka dhidi yake, inahusu ukiritimba aliouanzisha katika sekta ya Lychee. Mfanyabiashara huyo mkubwa alidhibiti mauzo ya nje kwa mkono wa chuma hadi aliposafiri kwenda Mauritius mwezi Oktoba mwaka uliyopita.

Uzalishaji wote wa lychee nchini Madagascar uliokusudiwa kusafirishwa nje ulinunuliwa awali “kwa bei nafuu” na kampuni iliyoko Mauritius, kitengo cha kupambana na ufisadi huko Antananarivo kimebainisha katika taarifa iliyotolewa siku ya Jumamosi. Kampuni ya shell, inayomilikiwa na Mamy Ravatomanga, kisha ikauza tena bidhaa hizo “kwa bei kubwa,” kulingana na mahakama maalum.

“Faida zote zinatokana na vitendo hivi vya siri na haramu,” kitengo cha kupambana na ufisadi kiliongeza katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, “kisha husafishwa kupitia makampuni kadhaa ya kundi la SODIAT, pamoja na makampuni mengine ya Mamy Ravatomanga.”

Kwa jumla, watu wanane na makampuni kumi na mawili wanashtakiwa kwa utakatishaji fedha, ufisadi, biashara ya ushawishi, upendeleo, na mgongano wa maslahi.

Mamy Ravatomanga tayari ana hati ya awali ya kukamatwa kwa jukumu lake katika uwasilishaji wa ndege za Boeing kwa siri kwa Iran.

Kesi yake inahusu ushirikiano wa karibu wa kimahakama kati ya Madagascar na Mauritius, ambazo zinafanya kesi tofauti. Anaweza tu kupelekwa Madagascar baada ya kushtakiwa nchini Mauritius, kama inavyotakiwa na mamlaka ya Madagascar.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *