• Mzee wa umri wa miaka 73 aliyetambulika kwa jina la Peter Kimani kutoka kaunti ya Nakuru anadaiwa kuuawa na muuaji aliyekodishwa na familia yake eneo la Bahati
  • Familia hiyo imekuwa na mizozo ya muda mrefu ya kifamilia kuhusu ardhi, hali iliyosababisha mama na watoto wake kupanga njama ya mauaji ya kikatili ya Peter Kimani
  • Wakazi walionyesha mshtuko kuhusu kuhusika kwa familia katika kifo cha baba yao, na pia walielezea jinsi alivyokuwa akiteswa kabla ya kifo chake

Nakuru, Kenya: Familia ya watu wanne imewashangaza wakazi wa Bahati kaunti ya Nakuru baada ya kudaiwa kula njama na kumwajiri muuaji ili kumuua baba yao.

bahti
Peter Kimani, aliyefariki (kushoto), wajukuu zake, ambao walikuwa miongoni mwa washiriki wa kwanza (kulia). Picha: NTV.
Source: Facebook

Katika taarifa iliyoshirikiwa kwenye runinga ya NTV Kenya, iliibuka kuwa mama mmoja na watoto wake walipanga njama ya kumuangamiza Peter Kimani siku ya Jumapili baada ya madai ya mzozo kuhusu ardhi.

Mmoja wa binti za Kimani, Joyce Wanjiru, alisema wafanyakazi wake hawakuweza kupata vifaa walivyohitaji, na mwanadada huyo alipoingia ndani ya nyumba hiyo, alimkuta babake akiwa amelala kwenye dimbwi la damu na kuanza kupiga nduru, ndipo alipogundua kuwa mzee huyo alikuwa amejeruhiwa vibaya kichwani.

Pia soma

Machakos: Familia Yalia Kumpoteza Binti Wao Aliyefariki katika Shule ya Bweni

“Tulimpeleka hospitali kwa haraka, lakini alifariki kwa masikitiko makubwa,” alisema jamaa wa karibu.

“Wakati tunalia nje ya nyumba, alitokea mwanamke huyo na watoto wake na kuanza kulia huku wakijifanya wanaomboleza baba yao, lakini hata machozi hayakuwatoka,” alidai mwanamke mwingine.

famili
Baadhi ya jamaa za Peter Kimani. Picha: NTV.
Source: Facebook

Je, Kimani alikuwa akishughulikiwa vipi hapo awali?

Polii walipata fimbo mbili za mbao zilizokuwa na damu zinazoaminika kutumika katika shambulio hilo.

Mjukuu wa marehemu alisema kuwa walikutana na marehemu, na alikuwa na mikwaruzo mkononi.

Walipomuuliza, alisema kwamba alikuwa amechanwa tu, lakini mtoto aliwaambia kwamba kuna mtu amemng’ata.

“Inadaiwa walijaribu kumnywesha sumu na kushindwa jambo ambalo lilimfanya aende kula chakula nyumbani kwa jamaa mwingine, wamekuwa wakigombana kwa muda mrefu kuhusu ardhi kwa kuuza ardhi na kila mtoto anataka kupata pesa,” alisema mjukuu huyo.

Maoni ya Wakenya kuhusu mauaji ya Kimani

Chirchir Kip: “Kwa wagikuyu hiyo si maajabu,other communities pray for their parents to live longer hawa wanaonanga aende awaachie shamba.”

Richard Sosi: “Pole.”

Meggie Spice: “Mbona yule bibi mwenye rangi nyekundu nyuma yako anakuja kucheka huko?”

Pia soma

Bintiye Ong’ondo Were amkumbuka babake katika ujumbe wa kugusa moyo

Lucie Mukora Kabena: “Inasikitisha sana … ni karma gani ya kuona itawafuata.”

Veronica Irungu: “Mbaya sana.”

Chirchir Kip: “Hiyo si maajabu, other communities pray for their parents to live longer hawa wanaona aende awaachie shamba.”

Mzee wa Miaka 25 Adaiwa kumuua Babake

Mnamo Januari 20, mzee wa miaka 56, Joel Kipyegon Kosgei, alidaiwa kuuawa na mtoto wake wa kiume, kutokana na mzozo wa ardhi katika nyumba yao huko Bomet.

Polisi wametoa taarifa ambayo ilithibitisha kuwa uchunguzi unaendelea huku wanakijiji wakimshambulia mshukiwa aliyetambulika kama Hillary Yegon baada ya tukio hilo baya.

Kulingana na Edward Imbwaga, kamanda wa polisi kaunti ya Bomet, maafisa wa upelelezi walipata silaha iliyokuwa na damu.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *