Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, amekaribisha ishara ya “kutia moyo” katika mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja na Marekani kuhusu mpango wa nyuklia wa amani wa Tehran lakini amesema Jamhuri ya Kiislamu iko tayario kwa “hali yoyote inayowezekana.”

“Mazungumzo ya karibuni [na Marekani] yalihusisha ubadilishanaji wa mapendekezo ya vitendo na kutoa ishara za kutia moyo,” Pezeshkian alisema katika ujumbe wake kwenye akaunti yake ya X jana Jumapili.

Amesisitiza kwamba Iran inaendelea kufungamana na amani na utulivu katika eneo la Magharibi mwa Asiala kini ameeleza kuwa Tehran inaendelea kufuatilia kwa karibu viitendo vya Marekani.

“Iran imefanya maandalizi yote muhimu kwa hali yoyote inayoweza kutokea”, amesema Rais Masoud Pezeshkian.

Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, alisema jana Jumapili kwamba duru mpya ya mazungumzo na Marekani inatarajiwa kufanyika mjini Geneva, Uswisi, siku ya Alkhamisi.

Araghchi katika mahojiano na CBS News

Katika mahojiano yake na CBS News, Araghchi amesema bado kuna “nafasi nzuri” ya kupatikana suluhisho la kidiplomasia kwa mzozo wa nyuklia kwa mujibu wa maslahi ya pande zote, akisisitiza: “Suluhisho linaweza kufikiwa.”

Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman, Sayyid Badr bin Hamad Al Busaidi baadaye alithibitisha kwamba mazungumzo hayo yatafanyika Alhamisi mjini Geneva.

Oman hapo awali ilikuwa mwenyeji wa mazungumzo ya nyuklia kati ya Iran na Marekani na imewezesha duru ya hivi karibuni ya mazungumzo hayo mjini Geneva, wiki iliyopita.

Ajenda ya mazungumzo ya awali huko Muscat na Geneva ilijikita zaidi katika suala la nyuklia na kuondolewa vikwazo haramu vya Marekani dhidi ya Iran.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *