Suala la Sahara Magharibi ndilo kiini cha duru mpya ya mazungumzo iliyoandaliwa Washington kuanzia Februari 23 hadi 24, 2026. Marekani inaongeza kasi. Wiki mbili baada ya mkutano wa awali uliofanyika katika ubalozi wa Marekani huko Madrid, Massad Boulos, mjumbe wa Donald Trump kwa Afrika, sasa anazileta pamoja Morocco, Algeria, Mauritania, na Polisario Front katika mji mkuu wa Marekani.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kikao hiki cha kidiplomasia cha faragha kinaonyesha ushiriki wa moja kwa moja wa Ikulu ya White House katika suala hili la karibu miaka hamsini. Lakini nyuma ya kasi hii, misimamo inaendelea kuwa tofauti sana kati ya Rabat, Polisario Front, na Algiers.

“Huu ni mkutano wa tatu katika kipindi cha mwezi mmoja, ambao unaonyesha kwamba Marekani inafanya kila iwezalo kujaribu kufikia matokeo, labda mwishoni mwa masika,” anaeleza mwandishi wa habari wa Uhispania Ignacio Cembrero, ambaye alifichua mikutano hii ya siri kwa mara ya kwanza, akizungumza na mwandishi wetu wa habari wa kitengo cha kanda ya Afrika, RFI Afrique, Christina Okello.

Kulingana na yeye, ushiriki huu una malengo kadhaa. “Donald Trump anataka kujionyesha kama rais wa amani, mtu anayefanikiwa kupata makubaliano kati ya maadui wa zamani, kama ilivyo kwa Morocco na Polisario Front, ambayo inapigania uhuru wa Sahara Magharibi, ambayo kwa sasa inadhibitiwa zaidi na Morocco.”

Motisha nyingine: kuisaidia Morocco, mshirika wa Marekani barani Afrika, “ambayo imejiunga na Baraza la Amani na hata itakuwa moja ya nguzo za kikosi cha utulivu ambacho Marekani inakianzisha Gaza.” Kwa hivyo Washington inatafuta “suluhisho zuri” kwa mshirika wake wa Morocco.

“Morocco ni nchi rafiki ambayo Marekani inataka kusaidia kwa kupata suluhisho linalofaa kwa mzozo wa Sahara Magharibi”, amesema Ignacio Cembrero, mwandishi wa habari wa jarida la Uhispania El Confidencial.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *