Mwishoni mwa juma rais wa Uganda, Yoweri Museveni, amekutana kwa mazungumzo na kiongozi wa wapiganaji wa RSF wa nchini Sudan, Mohamed Hamdan Gadalo, mjini Entebbe.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa tarifa iliyotolewa na ikulu ya Uganda, wawili hao walijadiliana kuhusu namna ya kumaliza mzozo unaoendelea na kuleta utulivu kwenye ukanda.

Katika mazungumzo yao rais Museveni alisisitiza maoni yake kuwa kwa mzozo wa nchi hiyo kupata Suluhu ya kudumu ni lazima kuwe na mazungumzo jumuishi kuliko nguvu za kijeshi.

Rais Museveni aliteuliwa na umoja wa Afrika kuongoza kamati maalumu itakayoratibu mkutano wa ana kwa ana kati ya Dagalo na kiongozi wa kijeshi Abdel Fattah al Burhan.

Mkutano huu ulikuwa wa Kwanza kwa Dagalo kuonekana hadharani tangu alipoonekana mara ya mwisho mwezi Juni mwaka uliopita katika mkanda wa vĂ­deo akizungumza na wapiganaji wake mjini Darfur.

Licha ya Dagalo kuonesha utayari wa kusitisha vita na kuruhusu misaada ya kibinadamu, hali ni tofauti kwa Al Burhan ambaye amesema hatasitisha vita hadi pale wapiganaji wa RSF watakapondoka kwenye miji wanayoishikilia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *