Afrika Kusini jana Jumatatu ilitoa wito kwa nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa kulitambua taifa la Palestina na kudhihirisha mshikamano na wananchi wa Palestina.

Ronald Lamola Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini alisema jana katika mkutano wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Uswisi kwamba nchi hiyo inaendelea kutoa wito ili kukomeshwa uvamizi na ukaliaji mabavu haramu wa Israel, kukomesha mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na utawala huo, na hatua zake za kuwahamisha kwa nguvu Wapalestina katika Ukanda wa Gaza na   Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

” Afrika Kusini inasisitiza uungaji mkono wake usioyumba na kutangaza mshikamano na wananchi wa Palestina,” amesema Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini.

Lamola pia amesema Afrika Kusini ina wasiwasi kuhusu mashambulizi dhidi ya Francesca Albanese Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina na pia baraza huru la wataalamu wa masuala ya haki za binadamu lililoteuliwa kusimamia, kushauri na kuripoti kuhusu hali mahsusi ya mambo ya nchi kwa ujumla. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini amesema nchi hiyo itatumia nafasi yake ya uanachama katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kupambana na aina zote za ubaguzi, ikiwa ni pamoja na tatizo la ubaguzi wa rangi , na kuendelea kuwawezesha wanawake n.k.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *