Chanzo cha picha, Getty Images
Tume ya Uchunguzi kuhusu matukio ya machafuko wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 imepewa siku 42 za ziada, kuanzia Ijumaa, Februari 20, 2026. Citizen imeripoti
Tume hiyo, iliyoteuliwa na kuzinduliwa na Rais Samia Suluhu Hassan, awali ilipewa siku 90 kukamilisha kazi yake.
Kipindi hicho kilianza Novemba 20, 2025 na kukamilika Februari 20, 2026.
Kulingana na taarifa iliyotolewa na tume hiyo, nyongeza ya siku 42 imeidhinishwa ili kutoa muda wa kutosha kukamilisha uchunguzi kuhusu matukio ya machafuko yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 29, 2025.
Kwa nyongeza hiyo, tume sasa inahitajika kukamilisha kazi yake na kuwasilisha ripoti yake mnamo au kabla ya Aprili 3, 2026.
Matukio yaliyoripotiwa katika maeneo kadhaa kote nchini yalijumuisha maandamano ambayo yaliongezeka na kuwa vurugu, na kusababisha vifo, majeraha na uharibifu wa miundombinu ya serikali na ya binafsi.
Mamia ya waandamanaji walikamatwa na kushtakiwa kwa uhaini.
Baadhi wamesamehewa na Rais Samia Suluhu Hassan, huku wengine wakiendelea kushtakiwa mahakamani.
Katika taarifa yake, tume ilitaja sababu kadhaa za kuongezwa kwa muda huo, ikisema kwamba muda huo wa ziada utatoa fursa kwa mtu yeyote, iwe ndani au nje ya nchi, ambaye ana taarifa, ushahidi au maoni ya kuwasilisha, kujitokeza. Tume ilisema lengo ni kuhakikisha kwamba hakuna mtu au taasisi inayonyimwa fursa ya kusikilizwa.
Unaweza kusoma;