
Takriban wanajeshi 10,000 walitumwa kote Mexico kufuatia kifo cha El Mencho, kiongozi wa Genge la Kizazi Kipya la Jalisco, katika operesheni ya kijeshi siku ya Jumapili, Februari 22. Vizuizi vya barabarani na mashambulizi yaliyohusishwa na kundi hilo la kihalifu yaliripotiwa katika karibu kila jimbo la Mexico, kabla ya kurudi kwa hali ya utulivu siku ya Jumatatu, Februari 23.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Karibu watu 60 walifariki, kulingana na ripoti ya awali ya serikali. Operesheni hii ina hatari kubwa ya kisiasa kwa Rais wa mrengo wa kushoto Claudia Sheinbaum.
Hatari ya kwanza: rais wa Mexico hajui ni kiasi gani kisasi cha genge hilo kitakuwa. Hatari nyingine: kifo cha Nemesio Oseguera, jina la utani El Mencho, kinaweza kugawanya shirika hilo na hata kusababisha vurugu zaidi kati ya wafanyabiashara wa dawa za kulevya na dhidi ya raia.
Hatimaye, serikali ya Mexico inaweza kushtakiwa kwa kuchukuwa hatua chini ya shinikizo kutoka Marekani, ambayo ilitenga zawadi ya dola milioni 15 kwa mtu yeyote atakayemkamata mfanyabiashara huyu wa fentanyl, mmoja wa watu muhimu zaidi barani Amerika.
“Vikosi vya Marekani havikushiriki katika operesheni hiyo”
Siku ya Jumatatu, Claudia Sheinbaum alidai kwamba hakuna mwanajeshi wa Marekani aliyeandamana na wanajeshi wa Mexico wakati wa operesheni hiyo.
Vikosi vya Marekani havikushiriki katika operesheni hiyo. Kilichotokea ni kubadilishana taarifa za kijasusi na Marekani: serikali ya Marekani ilitupatia taarifa. Lakini operesheni nzima, ikiwa ni pamoja na mipango yake tangu mwanzo, iliendeshwa na vikosi vya shirikisho vya Mexico, chini ya jukumu la Wizara ya Ulinzi wa Kitaifa.
Tofauti na mtangulizi wake
Kabla yake, rais wa zamani Andrés Manuel López Obrador aliahidi mazungumzo badala ya mapigano ili kupambana na ukosefu wa usalama. Sera hii ilishindwa. Kwa hivyo rais mpya, aliyechaguliwa mwaka wa 2024, anatafuta kujitenga na sera hio. Amejikita zaidi katika ujasusi na uratibu miongoni mwa vikosi vya usalama vya nchi hiyo.
Lakini licha ya kifo cha El Mencho, bado na safari ni ndefu kwa Serikali kabla ya kurejesha udhibiti wa eneo lote.