Waziri mkuu wa utawala wa kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu amesema juhudi zinaendelea kufanywa za kuunda kile alichokielezea kama “muungano” wa kikanda wa kukabiliana na kile alichokiita “mihimili ya Sunni na Shia”.

Kwa mujibu wa Bloomberg, Netanyahu ametoa matamshi hayo katika mkutano wa baraza la mawaziri kabla ya ziara ya Waziri Mkuu wa India Narendra Modi wiki hii.

Amesema mtandao huo wa miungano atakaoupendekeza utazijumuisha India, nchi za Kiarabu na Afrika, Ugiriki, Cyprus na nchi zingine za Asia.

Netanyahu amedai kuwa nchi hizo zina mtazamo mmoja wa maono ambao ni tofauti na kile alichokiita “mhimili wa Shia wenye msimamo mkali” na “mhimili unaoibuka wa Sunni wenye msimamo mkali”.

Waziri mkuu wa utawala wa kizayuni wa Israel ameendelea kudai kwamba, lengo ni “kuunda mhimili wa nchi zinazoona uhalisia, changamoto na malengo kwa namna moja, tofauti na mihimili yenye msimamo mkali, unaojumuisha mhimili wa Shia na mhimili wenye msimamo mkali wa Sunni unaoanza kujengeka”.

Amesema ushirikiano kati ya nchi hizo unaweza kuleta “faida kubwa” na “bila shaka utatoa dhamana ya nguvu na mustakabali wao”.

Kwa madai yake, Netanyahu ameongeza kwamba, ikiwa nchi hizo zitajiunga na muungano huo, ushirikiano kama huo untaweza “kutoa matokeo muhimu na kuhakikisha uthabiti na mustakabali wa Israel”…/

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *