
Nchi ya Ukraine, hivi leo inaadhimisha miaka minne tangu ivamiwe kijeshi na Urusi, maadhimisho yanayofanyika huku licha ya kupata uungwaji mkono kimataifa, baadhi ya washirika wake wamegawanyika.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Vita ya Ukraine inatajwa kuwa mbaya zaidi kushuhudiwa tangu kumalizika kwa vita ya pili ya dunia, huku juhudi za upatanishi zikiendelea kukutana na vikwazo.
Mpaka sasa maelfu ya raia na wanajeshi wa Ukraine wamepoteza maisha tangu vita hiyo kuanza februari 24 mwaka 2022, mamlaka za Kiev zikiendelea kusisitiza kuwa mwishowe nchi yao itapata ushindi.
Uvalizi wa Urusi kwa Ukraine umezidisha hofu ya kutokea kwa vita nyingine ya dunia, hasa wakati huu ambapo nchi za Ulaya zikitangaza kuongeza bajeti zao za ulinzi kwa kile zinasema kujiweka tayari kwa chochote kinachoweza kufanywa na Urusi.
Hata hivyo, wakati huu wito wa amani ukitolewa, nchi za Ulaya zimetangaza msaada zaidi wa ulinzi kwa Ukraine, ambapo mkuu wa sera za kigeni wa umoja huo, Kaja Kallas anasema hawataiacha nchi hiyo.
Mpaka kufikia sasa Urusi inadhibiti karibu asilimia 20 ya ardhi ya Ukraine, ambapo licha ya shinikizo la kimataifa, rais Vladmir Putin amesisitiza kuendelea na vita hiyo hadi atakapofikia lengo.