Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amemteua mwanadiplomasia wa Gabon Parfait Onanga-Anyanga kama Mwakilishi wake Maalum wa Afrika ya Kati na kaimu mkuu wa Ofisi ya kikanda ya Umoja wa Mataifa kwa Afrika ya Kati (UNOCA). Mwanadiplomasia huyo wa Gabon amechukua wadhifa wake siku ya Jumatatu, akisubiri uthibitisho au uteuzi wa mkuu mwingine wa UNOCA kuchukua nafasi ya Abdou Abarry kutoka Niger, ambaye muhula wake unaisha.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Libreville, Yves-Laurent Goma

Antonio Guterres amemtaka mwanadiplomasia huyo kuhudumu kama kaimu mkuu wa UNOCA, wadhifa uliokuwa ukishikiliwa na Abdou Abarry, ambaye muhula wake wa miaka mitatu unamalizika. Parfait Onanga-Anyanga ana uzoefu wa miaka 30 katika ngazi za kitaifa nchini Gabon, kikanda, na kimataifa.

Alijiunga na mfumo wa Umoja wa Mataifa (UN) miaka 28 iliyopita. Kwa miaka minne iliyopita, raia huyo wa Gabon amehudumu kama Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Umoja wa Afrika (AU), mwenye makao yake makuu Addis Ababa, Ethiopia. Kabla ya nafasi yake katika Umoja wa Afrika, aliongoza mfululizo MINUSCA, ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Pembe ya Afrika, yenye makao yake makuu nchini Kenya.

Akiwa mkongwe wa misheni zenye changamoto, Parfait Onanga-Anyanga aliratibu majibu ya Umoja wa Mataifa kwa mgogoro wa Boko Haram na pia aliongoza ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Burundi kuanzia mwaka 2012 hadi mwisho wa mwaka 2014, kipindi kilichotawaliwa na mvutano mkubwa na mamlaka ya Burundi.

Akiwa mkuu wa UNOCA, atasimamia mtaifa kumi na moja ya Afrika ya Kati, ikiwa ni pamoja na DRC na Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR). Bado haijabainika kama atakuwa na makao yake Libreville au Addis Ababa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *