Sudan imesema kuwa pendekezo lolote la kumaliza vita na wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) linapasa kuzingatia maslahi makuu ya nchi hiyo, mshikamano na umoja wa ardhi nzima ya nchi hiyo.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan imesema katika taarifa yake kuwa pendekezo au ubunifu wowote halimaanishi kuwa limekubaliwa au kuidhinishwa na serikali ya Sudan.”

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan imesisitiza kuwa: Mapendekezo yoyote ya kukomesha vita na kurejesha amani nchini humo yanapasa kuzingatia maslahi makuu ya nchi, usalama wa taifa wa Sudan, umoja wa ardhi yote ya  Sudan, mshikamano wa taasisi zake na mamlaka ya kujitawala ya nchi hiyo.

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan imesisitiza kuwa Sudan ni nchi huru na inachukua maamuzi na misimamo kwa mujibu wa maslahi yake ya kitaifa. 

Massad Boulos mshauri wa ngazi ya juu wa Marekani nchini Sudan awali alkuwa amependekeza mkakati wa nguzo tano ilikuhitimisha vita huko Sudan.

Boulos alisema katika hotuba yake katika kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba Washington inashirikiana na pande nyingine washirika zikiwemo Misri, Saudi Arabia, Imarati na Uingereza kushinikiza kufikiwa mapatano ya kusitisha vita nchini Sudan bila ya masharti. 

Sudan imetumbukai katiak vita vya wenyewe kwa wenyewe vya kuwania madaraka tangu Aprili 2023 ; vita ambavyo  hadi sasa vimeuwa makumi ya maelfu ya Wasudani na kupelekea wengine wasiopungua milioni 13 kuwa wakimbizi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *