MWANZA; Taasisi ya Doris Mollel Foundation chini ya Mkurugenzi Mtendaji wake Doris Mollel, imefanikisha ujenzi wa jengo jipya la kisasa maalumu la kwanza nchini kwa ajili ya kutoa huduma bora kwa watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (watoto njiti) lililopo katika Hospitali ya Wilaya ya Kwimba, mkoani Mwanza.

Jengo hilo lenye thamani ya Sh bilioni 2.125 linatarajiwa kuzinduliwa rasmi Februari 28, 2026 na Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dk Tedros Adhanom Ghebreyesus.

Jengo hilo limejengwa kwa ushirikiano na Taasisi ya Msanii maarufu wa Marekani, Alicia Keys inayoitwa Keep a Child Alive na lina chumba maalumu pia kwa ajili ya baba kumuona mama na mtoto wake akiwa hospitalini hapo na lina uwezo wa kuhudumia watoto 42 kwa wakati mmoja.

Mollel amesema baada ya kukamilisha ujenzi Kwimba, Taasisi hiyo itajenga majengo kama hayo kwenye mikoa mingine ikiwemo Dar es Salaam, Wilaya tatu za Mwanza, wilaya mbili za Shinyanga na Geita, Tabora pamoja na Zanzibar ambapo lengo ni kuwa na majengo 10 hadi kufikia mwaka 2028.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *