Wafungwa  wa kisiasa zaidi ya 30 wameachiliwa siku ya Jumatatu, Februari 23, kutoka gereza la Rodeo 1 nje kidogo ya mji mkuu wa Venezuela, Caracas, chini ya sheria ya msamaha iliyotangazwa Alhamisi chini ya shinikizo la Marekani baada ya kukamatwa kwa rais Nicolas Maduro mnamo Januari 3, waandishi wa habari wa AFP wameripoti.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Tuko huru, tuko huru!” walipiga kelele wafungwa, vichwa vyao vikiwa vimenyolewa na wamevaa fulana nyeupe, walipokuwa wakikaribishwa na jamaa wengi waliokuwa wamepiga kambi nje ya gereza kwa wiki kadhaa. Wafungwa walitoka mmoja baada ya mwingine.

Shirika lisilo la kiserikali la Foro Penal, ambalo lina utaalamu katika kuwatetea wafungwa wa kisiasa, liliripoti siku ya Jumatatu asubuhi kwamba watu 65 waliachiliwa huru katika siku tatu zilizopita chini ya sheria ya msamaha. Watetezi wa haki za binadamu wameona sheria hiyo haitoshi. Kwa mfano, haishughulikii kesi zinazohusiana na jeshi, ambazo hupatikana mara kwa mara katika gereza la Rodeo 1, ambapo wafungwa zaidi ya 200 walianza mgomo wa kula mwishoni mwa wiki iliyopita wakielezea upinzani wao. Baadhi ya wale walioachiliwa huru siku ya Jumapili na Jumatatu walikuwa miongoni mwa wale waliokuwa wametengwa na msamaha huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *