
wanamgambo wanaoiunga mkono serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamedai kuwa wamewauwa wapiganaji 50 waliokuwa wanachama wa kundi la waasi wa M23 na kuwateka nyara kadhaa katika mapigano makali hivi karibuni.
Kundi hilo lenye mfungamano na serikali ya Kinshasa kwa jina la Wazalendo limesema kuwa mapigano hayo yalijiri tarehe 16 na 22 mwezi huu wa Februari.
Limesema kuwa wapiganaji wake waliyateka maeneo kadhaa huko Masisi, Rutshuru na Walikale katika jimbo la Kivu Kusini na pia Fizi huko Kivu Kaskazini kufuatia mapigano kati yao na muungano wa waasi wa M23.
Taarifa ya kundi la wapiganaji la Wazalendo imeeleza kuwa wapiganaji wake wameyataja maeneo kadhaa huko Mutuza, Kasasa, Nkokwe na Kanyaru na hivyo kuwarudisha nyuma wapinzani wake katika umbali wa zaidi ya kilomita 10 kutoka katika mji muhimu kwa madini wa Rubaya.
Kundi la Wazalendo pia limenasa silaha nyepesi na nzito kutoka kwa waasi wa M23.
Hadi sasa waasi wa M23 hawatoa taarifa yoyote kuhusu madai haya ya kundi hilo lenye mfungamano na serikali ya Kinshasa.
Mapema jana Lawrence Kanyuka Msemaji wa waasi wa M23 aliituhumu Kinshasa kuwa imekiuka usitishaji vita mara kadhaa na kufanya ya mara kwa mara na ya kiholela katika maeneo yenye wakazi wengi hukoRumbishi.”
Wakati huo huo duru za habari za ndani zimearifu kuwa kundi la Wazalendo lenye mfungamano na serikali ya Kinshasa pia limeidhibiti tena mji wa Kasenyi, Chugi na Kinigi katika eneo la Masisi karibu na Rubaya.
Miji hiyo iliyoangukia mikononi kwa kundi la Wazalendo ilikuwa maeneo ya kimkakati ya muungano wa waasi wa AFC/M23 huko Masisi kwa sababu ya ukaribu wake na Rubaya.