
Maafisa wa ujasusi wa Israel wanakadria kuwa Marekani inaweza kuendeleza mashambulio ya kijeshi kwa “siku nne hadi tano” pekee dhidi ya Iran ikiwa itaanzisha uvamizi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu. Hii ni ka mujibu wa ripoti mpya.
Gazeti la Financial Times limetoa ripoti hii kwa kumnukuu afisa wa Israel ambaye amesema kuwa Marekani inaweza kufanya mashambulizi makali ya anga dhidi ya Iran yatakayodumu kwa “siku nne hadi tano tu,” au kutekeleza mashambulizi ya kiwango cha chini sana kwa takriban wiki moja.
Likinuuu duru za ujasusi, gazeti la Financial Times limeongeza kuwa: Hata kwa kutumwa shehena ya ndege ya USS Gerald R. Ford na kundi lake la mashambulizi katika eneo hili, uwezo wa Washington wa kutekeleza mashambulizi ya muda mrefu dhidi ya Iran utaendelea kuwa mdogo.
Financial Times limesema kuwa maafisa wa ujasusi wa Israel pia wametahadharisha kuwa mzozo wowote wa aina hii utakuwa na madhara kwa Marekani na pia kuiathiri pakubwa kisiasa serikali ya Rais Donald Trump wa Marekani.
Ripoti hii imetolewa huku serikali ya Trump ikiendelea kutuma zana za kivita katika eneo la magharibi mwa Asia. Rais wa Marekani ameendelea kukariri vitisho vyakek dhidi ya Iran na kuonya kuwa siku mbaya itashuhuhiwa iwapo hakutafikiwa makubaliano katika mazungumzo yanayoendelea ya nyuklia na Tehran.
Washington imeendeleza kampeni yake ya “mashinikizo ya kiwango cha juu” huku ikiimarisha uwepo wake wa kijeshi katika eneo la Asia Magharibi, ikiwa ni pamoja na kandokado ya Iran, kwa kutuma manowari mbili za kubebea ndege za kivita pamoja na ndege nyingi za kivita na mitambo ya makombora.
Wakati huo huo, duru ya tatu ya mazungumzo kati ya Washington na Tehran imepangwa kufanyika kesho Alhamisi huko Geneva Uswisi.
Hivi karibuni Meja Jenerali Amir Hatami Kamanda Mkuu wa Jeshi la Iran alibeza madai ya maadui ya kutoshindwa; na kusema kuwa maadui hawakutarajia kuiona nchi hii ikionyesha umadhubuti wake mbele ya kuendelea kukusanya majeshi katika kanda hii.