Dar es Salaam. Mwigizaji wa tamthilia ya Juakali, Heleina Herman ‘Love Juakali’ ameweka wazi kilichofanya aingie gym rasmi na kuanza kufanya mazoezi.
Mapema wiki hii mwigizaji huyo kupitia ukurasa wake wa Instagram, alichapisha video ikimuonesha akiwa gym anafanya mazoezi. Chapisho ambalo limewavutia mashabiki wengi huku wakimpongeza kwa uamuzi huo.
Akizungumza na Mwananchi, Love ameweka wazi kuwa hafanyi mazoezi kwa ajili ya kupunguza mwili kama wengi wanavyodhani.
“Am doing for funny, siwezi kupunguza mwili. Kwasababu mwili wangu ndio brand yangu kwahiyo nafanya tuu mazoezi ya kawaida ‘Physical fit and for funny’,”amesema Love
Love amesisitiza kuwa siyo mazoezi tu ya kupunguza mwili, hata kufanya upasuaji wa kupungua hawezi na hajafikiria kuufanya.
“Kwanini nifanye upasuaji wa kupunguza mwili. Wakati mwili wangu ndio brand yangu, kwahiyo sijawahi kabisa kufikiria kufanya upasauaji wa kupunguza mwili,”amesema Love Juakali
Mwigizaji huyu maarufu ametoa wito kwa wanawake kujiamini na kujikubali walivyo
“Wito wangu kwa wanawake ambao hawajiamini niseme tuu Mungu awatie nguvu. Kwasababu kujiamini ndio kunaweza kukufikisha popote hapa duniani,” amesema