#HABARI: Maafisa wa Kurugenzi ya Upelelezi nchini Kenya (DCI) wanamsaka Afisa wa Polisi anayeishi katika Kaunti ya Busia kwa tuhuma za kuhusika na tuhuma za mauaji ya mkewe waliyeachana katika hoteli moja iliyoko Silibwet Trading Centre, Kaunti ya Bomet.

Kwa mujibu wa Afisa wa Upelelezi wa Jinai katika Kaunti ya Bomet, Emmanuel Ogao, afisa huyo anadaiwa kumshawishi mwanamke huyo aende hadi hotelini, baada ya kumwambia kuwa anataka wasuluhishe mvutano wao, ndipo akachukua chumba katika hoteli na anadaiwa kumnyonga hadi kufa kabla ya kuutelekeza mwili wake katika eneo la tukio.

Polisi wanasema kuwa mshukiwa huyo alidaiwa kuwapigia simu baadhi ya jamaa zake, ili kuwafahamisha kuhusu tukio hilo, jambo lililosababisha tahadhari iliyopelekea maafisa kufika eneo ambalo mwili huo uligunduliwa.

Chanzo kimoja kilisema kuwa marehemu, ambaye ni mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Junior (JSS) kutoka eneo la Olenguruone Kaunti ya Nakuru, alikuwa akiishi na wazazi wake huko Bomet baada ya kuachana na mumewe huyo akidai ilikuwa ni ndoa isiyokuwa na afya kwake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *