#HABARI: Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekabidhi jumla ya magari 70 yenye lengo la kuongeza ufanisi na kurahisisha zoezi la ukusanyaji wa kodi nchini.
Katika shehena hiyo ya magari, yapo magari mawili ya kipekee ambayo yameundwa kama ofisi zinazotembea, yakilenga kuwafuata walipakodi katika maeneo yao na kutoa huduma kwa urahisi zaidi bila walipakodi kuhitaji kufika katika ofisi za kudumu.
Hatua hii ni sehemu ya mikakati ya mamlaka hiyo katika kuboresha mazingira ya kazi kwa watumishi na kusogeza huduma za kikodi karibu na wananchi, hususan katika maeneo ya mbali.
Ofisi hizo zinazotembea zinatarajiwa kupunguza msongamano maofisini na kuongeza hamasa ya ulipaji kodi kwa hiari, huku magari mengine yakisaidia katika doria na ufuatiliaji wa sheria za kodi ili kuhakikisha mapato ya serikali yanalindwa na kukua.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.