#HABARI: Zoezi la upimaji wa viwanja katika Mtaa wa Vikawe Shule, eneo la Butiama wilayani Kibaha, limeanza rasmi baada ya kumalizika kwa mgogoro wa muda mrefu kati ya wananchi na mmiliki wa eneo hilo.
Hatua hiyo, inayotekelezwa chini ya usimamizi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, imepokelewa kwa furaha na wakazi wa eneo hilo ambao wameeleza kuwa itawawezesha kuanza taratibu za kulipia maeneo yao na kupata hati miliki halali, jambo litakalomaliza hofu ya kupoteza makazi yao.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Vikawe Shule, Bw. Shabani Shabani, amesema kuwa anasimamia zoezi hilo kwa maelekezo ya Mkuu wa Wilaya ili kuhakikisha kila mwananchi anapata haki yake na kuepusha migogoro mipya hapo baadaye.
Wananchi wa Vikawe wameipongeza serikali kwa kuingilia kati suala hilo, wakibainisha kuwa upimaji huo ni ukombozi utakaosaidia kuleta utulivu na kuchochea maendeleo ya makazi katika mtaa huo uliokuwa na changamoto za umiliki kwa miaka mingi.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.