- Jacque Maribe alisherehekea siku ya kuzaliwa ya 72 ya marehemu babake kwa heshima kubwa kwenye mitandao ya kijamii
- Alitafakari jinsi alivyokuwa na furaha wakati wa siku yake ya kuzaliwa ya 71, akielezea huzuni ya kusherehekea mwaka huu bila uwepo wake
- Mtangazaji huyo wa zamani alisema alimpa mwanawe jina la babake ili kudumisha urithi wake, huku watu mitandaoni wakimfariji
Mtangazaji wa zamani wa Citizen TV, Jacque Maribe, bado anaendelea kukabiliana na majonzi ya kumpoteza babake, Maribe Mwangi.

Source: Instagram
Mzee Maribe alifariki dunia siku chache kabla ya Krismasi mwaka jana, jambo lililotia huzuni katika kipindi ambacho familia ilikuwa inatarajia kusherehekea.
Jacque aliwahi kufichua kuwa babake alipambana na saratani kwa muda mrefu kabla ya kufariki.
Jacque Maribe alimkumbukaje babake siku ya kuzaliwa?
Zaidi ya mwezi mmoja baada ya kumzika, mwandishi huyo mwenye majonzi aliingia kwenye Instagram kuadhimisha kile ambacho kingekuwa siku ya kuzaliwa ya 72 ya babake.
Alishiriki picha yake akiweka shada la maua kwenye kaburi la babake wakati wa mazishi, akitafakari jinsi mwaka huu ulivyo tofauti na uliopita.
Jacque alikumbuka jinsi yeye na binamu zake walivyomfanyia babake sherehe ya kushtukiza katika siku yake ya kuzaliwa ya 71, akieleza furaha ya kweli aliyokuwa nayo.
“Ulikuwa na furaha ya kweli wakati kama huu mwaka jana, ukiwa umezungukwa na watoto wako wengi. Mwaka huu, nilichobaki nacho ni kumbukumbu. Nakusherehekea kwa moyo wangu wote. Heri ya siku ya kuzaliwa ya mbinguni,” aliandika.
Jacque alieleza kuwa ataendelea kuheshimu na kuendeleza urithi wa babake, hasa kwa kuwa alimpa mwanawe jina lake.
“Nina furaha kuwa nilimwita mwanangu Maribe. Urithi wako unaendelea kuishi. Mwanangu anaweza kupata nguvu kutoka kwangu, lakini ukweli ni kwamba yeye ndiye anayeniweka imara sasa. Ulikuwa shabiki wake nambari moja, naye wako. Cheza na malaika kwa niaba yetu, Baba,” aliongeza.
Mtangazaji huyo aliyeguswa na huzuni pia alishiriki picha ya kugusa moyo ya babake marehemu akitembea sambamba na mjukuu wake, jambo lililowahuzunisha na kuwagusa wafuasi wake.
Wakenya wamtia moyo
Ujumbe wake wa hisia ulizua jumbe nyingi za faraja na maombi kutoka kwa mashabiki na marafiki zake, wakimtia moyo aendelee kuwa na nguvu katika kipindi hiki cha maombolezo.

Pia soma
Kizaazaa huku familia ikikataa kumruhusu mjane kuandaa maombi ya baada ya mazishi ya mume aliyeuawa
Baadhi ya jumbe hizo ni:
- Bettie S. Joseph: “Ulikuwa na baba wa kipekee kweli. Pole sana.”
- Grace Njuguna: “Baba aliyekuwa akimshika mkono hata mahakamani… ni maumivu makali. Apumzike kwa amani.”
- Nancy Keles: “Pole sana Jacky, dunia haina huruma. Jipe moyo.”
- Ziporah Njogu: “Pole kwa msiba. Mungu awatie nguvu.”

Source: Instagram
Je, Jackie Matubia anachumbiana na Dennis Itumbi?
Katika habari nyingine, Mkuu wa Miradi Maalum ya Rais na Uratibu wa Uchumi wa Ubunifu, Dennis Itumbi, alizungumzia uvumi kuhusu madai ya kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na Jacque Maribe.
Alikanusha uvumi huo wa muda mrefu kuwa walikuwa wanachumbiana, ingawa alifichua kuwa mamake aliwahi kutamani wawili hao wangeishia kuwa pamoja.
Hapo awali, wawili hao waliwahi kuzua gumzo mitandaoni baada ya picha yao wakibusiana kusambaa, jambo lililochochea zaidi tetesi za uhusiano wao.
Read ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.
Chanzo: TUKO.co.ke
