
Marekani na Saudi Arabia zinaripotiwa kushinikiza kuahirishwa kwa uchaguzi wa wabunge uliopangwa kufanyika mwezi Mei nchini Lebanon, huku Hezbollah na Waziri Mkuu wa zamani Saad Hariri wakiendelea kuwa maarufu.
Imechapishwa:
Dakika 3 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Beirut,
Wakati Waziri Mkuu wa zamani Saad Hariri alipopendekeza mnamo Februari 14 kwamba uchaguzi ujao wa bunge huenda usifanyike kama ulivyopangwa kufanyika mwezi Mei, matamshi yake yalisababisha msukosuko nchini Lebanon. “Ikiwa uchaguzi utafanyika, watasikia na kuhesabu kura zetu,” aliwaambia wafuasi wake wakati wa hotuba katikati mwa jiji la Beirut, wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 21 ya kuuawa kwa baba yake, Rafik Hariri.
Siku chache baadaye, mashaka yaliyotolewa na kiongozi huyo wa Kisunni yalithibitishwa na Nabih Berri, kiongozi mkuu wa Kishia nchini humo. Spika wa Bunge, mtu wa kwanza kuwasilisha rasmi ugombea wake wa uchaguzi, alibainisha mnamo Februari 15 katika taarifa iliyotolewa kwa Gazeti la kila siku la Saudi Arabia Al-Sharq al-Awsat kwamba “kauli ndani ya ‘kundi la nchi watano’ inaunga mkono kuahirishwa kwa uchaguzi.”
“Kundi la nchi watano” ni mfumo usio rasmi wa uratibu wa kidiplomasia, ulioundwa mwaka wa 2023, ukizileta pamoja nchi tano zenye ushawishi zinazohusika katika kusimamia mgogoro wa kisiasa na kitaasisi wa Lebanon: Marekani, Ufaransa, Misri, Saudi Arabia, na Qatar.
“Niliwafahamisha mabalozi kuhusu kupinga kwangu kuahirishwa kwa uchaguzi wowote na kuongeza mamlaka ya Bunge la sasa,” Nabih Berri aliongeza kwa gazeti hilo. Rais Joseph Aoun pia alielezea kujitolea kwake kufanya uchaguzi katika tarehe iliyopangwa. Katika ujumbe uliochapishwa kwenye mitandao ya kijamii mnamo Februari 3, ofii ya rais wa Lebanon ilithibitisha “uamuzi” wake wa kufanya uchaguzi wa wabunge “kuanzia Mei 3.”
Bunge, taasisi mama ya mfumo wa madhehebu
Siku nne mapema, Wizara ya Mambo ya Ndani ilichapisha orodha za uchaguzi, hivyo kuzindua maandalizi ya kiutawala kwa ajili ya uchaguzi wa bunge, tukio muhimu zaidi la kikatiba nchini.
Nchini Lebanon, Bunge ndilo taasisi mama. Linamchagua Rais wa Jamhuri, linamteua Waziri Mkuu, na kupitisha sheria. Ni ndani ya Bunge ambapo usawa maridadi wa mfumo unaojulikana kama “udini wa kisiasa” unaonyeshwa, kulingana na usambazaji wa kidini wa kazi zote za serikali.
Kwa hivyo, nia ya kisiasa ya kupanga uchaguzi kulingana na kalenda ya kikatiba ilionyeshwa wazi katika ngazi ya juu, na maandalizi ya kiutawala yakaanza. Kwa nini uchaguzi usifanyike?
“Kuna muunganiko wa maslahi kati ya Marekani na Saudia Arabia kuahirisha uchaguzi,” chanzo cha kisiasa kinachodai kutotajwa jina kimesma. Matamshi haya yanathibitishwa na wajumbe wa serikali ambao waliiambia RFI kwamba masuala muhimu yanahusu “ujumuishaji wa hali halisi mpya za kisiasa” zilizoibuka baada ya vita vya mwisho kati ya Hezbollah na Israel.
“Baada ya vikwazo vikubwa vilivyowapata Hezbollah na vuguvugu hili linlaounga mkono Iran, Marekani na Saudi Arabia wameunda upya tawi la utendaji linalowapendelea,” chanzo hicho cha kisiasa kinaeleza. “Walimfanya Joseph Aoun achaguliwe kuwa rais na kumteua Nawaf Salam kuwa mkuu wa serikali. Hata hivyo, katika Bunge, Hezbollah na washirika wake wanabaki kuwa na nguvu na wana nguvu ya kuzuia sheria, hata kama bado hawajaitumia. Ili kuendeleza ushawishi wa Marekani na Saudi Arabia, hali halisi ya kisiasa baada ya vita lazima ibadilishwe kuwa usawa mpya wa nguvu katika Baraza la Wawakilishi.”
Kwa hivyo, hali ya sasa nchini Lebanon haingeruhusu mabadiliko makubwa katika usawa wa madaraka uliopo ambao ungeunda mkondo mpya unaofaa zaidi kwa mhimili wa Marekani na Saudi Arabia.
Katika bunge la sasa, linaloundwa na wajumbe 128, lenye idadi sawa ya Wakristo na Waislamu, Hezbollah na mshirika wake, Harakati ya Amal ya Nabih Berri—inayojulikana kama kundi la Kishia—wana ukiritimba kamili juu ya uwakilishi wa Shia. Viti 27 vilivyotengwa kwa ajili ya jumuiya hii vilishindwa na wagombea wao katika uchaguzi wa mwaka 2022. Hii iliwaruhusu kudumisha urais wa Bunge, ambao umepewa Shia na Katiba na ambao Nabih Berri ameushikilia kwa miaka 34.”
Licha ya vita na shinikizo, Hezbollah inasalia kuwa maarufu
Jumuiya ya Washia ndiyo iliyoathiriwa zaidi na vita na Israel (Oktoba 8, 2023 – Novemba 27, 2024), haswa wakati wa siku 66 za mwisho za mzozo. Kwanza kabisa, kulikuwa na hasara za watu, huku maelfu wakiuawa na kujeruhiwa.