
Mapigano makali yameripotiwa kati ya wapiganaji Wazalendo, wanaoshirikiana na jeshi la Congo, na waasi wa kundi la M23/AFC katika maeneo ya Masisi mkowa wa Kivu kaskazini na Kalehe mkowani Kivu Kusini Mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia hapo jana, vyanzo kadhaa vimethibitisha.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya ndani na mashirika ya kiraia katika eneo la Kalehe, mapigano ya Jumatano yamejikita katika kijiji cha Kasenyi, eneo la Kibabi ya kwanza, na huko Mahanga, eneo la Nyamaboko, ambako Waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wanaripotiwa kuanzisha mashambulizi baada ya vikosi vya serikali kuyadhibiti tena maeneo kadhaa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Radio ya umoja wa mataifa, Okapi, tangu alfajiri ya jana, Mapigano hayo yaliendelea katika eneo la Butsike, na kwamba muungano wa wapiganaji Wazalendo kwa kushirikiana na FARDC, ulikuwa tayari umeviteka vijiji vya Kazinga na Ndete.
Aidha mashirika ya kiraia katika eneo la Masisi yanasema waasi hao wanajaribu kuzuia kusonga mbele kwa vikosi vinavyounga mkono serikali kuelekea mji wa madini wa Rubaya, huku Wakazi wengi wa Kazinga, Ndete, Chugi, Kaniro, na maeneo jirani wakiwa tayari wamekimbia vijiji vyao.